Serikali imeshindwa kupata waombaji wenye sifa katika kada
za wahandisi vifaa tiba, maofisa wauguzi ngazi ya shahada, wataalam wa mionzi,
madaktari wa meno na watalaam wa viungo bandia
Akizungumza leo Jumatatu Juni 9, 2018 Waziri wa Nchi Ofisi
ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo
amewataka wananchi kusomea taaluma hizo kwa kuwa mahitaji ni makubwa mno
“Katika mchakato imebainika kuwapo tatizo la ucheleweshaji
wa utoaji wa vyeo vya kitaalam kwa wahudumu katika baadhi ya vyuo na Baraza la
Taifa la Elimu ya Ufundi (Nacte)," amesema
Amesema jumla ya waombaji 3,440 wengi wao wakiwa
waliomaliza vyuo mwaka 2016/17 walishindwa kuwasilisha vyeti vya Nacte
katika maombi yao ya ajira na kufanya baadhi ya kada kukosa waombaji wenye sifa
wa kutosha ikilinganishwa na mahitaji ya Tamisemi
"Ofisi ya Rais Tamisemi imefanya mawasiliano na Nacte
ili kuharakisha mchakato wa utoaji vyeti utakaowawezesha wahitimu wote wenye
sifa kuweza kuajiriwa," amesema
Serikali yaeleza ilivyoshindwa kupata watumishi wenye sifa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 09, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 09, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment