WADAU wanaojishughulisha na ununuzi wa mazao mbalimbali
mkoani hapa wamewataka wakulima kuacha tabia ya kuchanganya nafaka
na mchanga kwa kuwa hali hiyo imekuwa ikiondoa ubora na thamani wa
mazao
Ushauri huo ulitolewa na Meneja wa kiwanda cha The Agro
Processing Africa Purimui Suvuiiyu baada ya kubainika baadhi ya wakulima
wa zao la choroko kuwa na tabia ya kuchanganya nafaka na mchanga kwenye
magunia kwa lengo la kuongeza uzito
Akizungumza na waandishi wa habari mbele ya wanunuzi wakuu
wa nafaka kutoka kampuni ya Export Trading LTD yenye makao makuu ya jijini Dar-
es- salaam, meneja huyo alisema kuwa baadhi ya wakulima wamekuwa wakiongeza
uzito kwa kuchanganya kwenye nafaka hizo kwa kuweka mchanga
Alisema hali imekuwa ikishusha thamani ya zao hilo
“Kiwanda chetu kinajishughulisha na shughuli za uchakataji
wa choroko ambazo tunanunua kutoka kwa wakulima, kinachosikitisha baadhi yao
siyo waaminifu wamekuwa wakichanganya mchanga na nafaka zingine ambazo siyo za
choroko na kusababisha kiwanda kuingia kwenye hasara kubwa,”alisema.
Alisema kuwa kiwanda hicho kinauza choroko zake hadi nchi za
nje hivyo kitendo cha wakulima kuchanganya zao hilo na vitu vingine vinaweza
kushusha thamani kwenye masoko ya nje ambao wamekuwa
wakinunua
Naye, Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Export
Trading Group, Fatuma Ally alisema choroko inayonunuliwa toka kwa wakulima wadogo
wakati mwingine inakuwa haina ubora wa kutosha na kutokidhi vigezo kwenye
masoko ya nchi za nje
Alisema hukutwa choroko zimechanganywa na mchanga hivyo
kusababisha ufanyaji wa kazi kubwa wa usafishaji kabla ya uchakataji na pia
kupunguza kiwango cha choroko iliyonunuliwa
Hata hivyo alisema kwa upande wao wa kampuni ya Export
imekuwa ikinunua mazao mbalimbali kwa ajili ya kuwakomboa wakulima katika
kujipatia kipato cha bei pamoja na soko
Waonywa kuchanganya nafaka na mchanga
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 28, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 28, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment