Wakati Tanzania kesho ikiungana na nchi nyingine duniani
kuadhimisha siku ya kupinga usafirishaji binadamu, wadau kutoka serikalini na
taasisi binafsi wamekutana kujadili namna ya kufanya udhibiti
Mkutano umefanyika leo Julai 29, 2018 ukiangazia hali halisi
ya biashara ya usafirishaji binadamu Tanzania, changamoto za kisera na kisheria
zilizopo na namna ya kuzitatua
Katibu wa sekretarieti ya kupambana na usafirishaji wa binadamu,
Seperatus Fella amesema Julai 30 ya kila mwaka ni siku ya kupinga biashara ya
usafirishaji binadamu wameona ni vyema kukutana kitaifa kujadili mambo kadhaa
kuhusu janga hilo
Amesema upungufu katika sheria zilizopo ni miongoni mwa mada
zilizochukua nafasi katika mkutano huo, wadau wakisema udhaifu huo unapunguza
weledi na juhudi zilizopo
"Serikali inatarajia kufanya marekebisho ya sheria ya
kudhibiti biashara ya usafirishaji wa binadamu ya mwaka 2008 ili kuiongezea
makali," amesema Fella
Mratibu wa mradi wa kupinga biashara ya kusafirisha binadamu
unaosimamiwa na shirika la kimataifa la RTI, Edwin Mugambila amesema sheria
iliyopo ina upungufu na hasa katika vipengele kuhusu njia za usafirishaji wa
binadamu na hukumu kwa wanaojaribu kusafirisha binadamu lakini wakashindwa
Amesema pia sheria haitoi maelekezo kuhusu hatima ya
walioathiriwa na usafirishaji wa binadamu
"Sheria bado haikidhi vigezo vya kukomesha biashara hii
hatari, tunahitaji mabadiliko," amesema
Amesema adhabu zinazotolewa kwa wanaokamatwa bado haitoshi
kukomesha biashara hiyo
Mugambila amesema sheria hutoa hukumu ya kifungo cha hadi
miaka 10 jela au faini ya Sh150 milioni
Wadau wataka udhibiti zaidi usafirishaji binadamu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 29, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 29, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment