Lugola atishia kufuta makanisa, misikiti yenye migogoro


Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema hatasita kufuta makanisa au misikiti inayoshindwa kutatua migogoro ya taasisi hizo

Ametoa kauli hiyo leo katika Kanisa la Pentekoste la Leganga, lililopo Arumeru mkoani Arusha Ambapo Amesema Kuanzia sasa, kanisa lolote au msikiti wowote utakaokumbwa na migogoro na kushindwa kuitatua wenyewe; misikiti hiyo, makanisa hayo nitakwenda kuyafuta mara moja

Amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha yanakuwapo makanisa na misikiti inayohubiri amani na utulivu.

Waziri Lugola ameonya askari Polisi wanaowashusha jukwaani masheikh na wachungaji inapofika saa 12:00 jioni, akisema muda huo ukifika waimarishe ulinzi ili waumini wamalize ibada zao vizuri
Lugola atishia kufuta makanisa, misikiti yenye migogoro Lugola atishia kufuta makanisa, misikiti yenye migogoro Reviewed by KUSAGANEWS on July 29, 2018 Rating: 5

No comments: