Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ameagiza uongozi wa
chama hicho kila wilaya kujenga ofisi ifikapo mwaka 2020 na kuondokana na
kupanga
Mbowe amesema hayo leo wakati akiweka jiwe la msingi katika
jengo la ofisi ya Chadema wilayani Tarime mkoani Mara
Mwenyekiti huyo baada ya kukagua jengo la ofisi hiyo lenye
vyumba vitatu, amesema mpango wa ujenzi wake ulicheleweshwa lakini akawapongeza
viongozi walioona njozi ya kuanzisha ujenzi huo ambao uko hatua ya renta
"Mimi naanza na Sh2 milioni kila mbunge mkoani Mara
achangie milioni moja," amesema Mbowe
Wabunge na wenyeviti wa halmashauri wamefikisha Sh10 milioni
"Shughuli hii itasimamiwa na katibu wa chama mkoa,
Chacha Heche ambaye ndiye mratibu wa mambo yote ya chama mkoa," amesema
Awali, mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Tarime, Lucas Ngoto
akitoa taarifa fupi kuhusu upatikanaji na ujenzi wa jengo hilo la ofisi
amesema: "Tulinunua uwanja huu mwaka 2012 kwa Sh6 milioni, lakini likiwa
na mgogoro ambao uliisha baadaye
“Mwaka huu mwezi wa pili tulianza ujenzi na kufikia hapa
baada ya kukosa fedha ndani ya chama na fedha nyingine kutolewa na mbunge (wa
Tarime Mjini), Esther Matiko, ili kukamilisha ujenzi huu tunahitaji Sh7
milioni, " amesema Ngoto
Mbowe ataka kila wilaya kujenga ofisi kabla ya 2020
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 29, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 29, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment