Magufuli amteua Jokate Mwegelo Mkuu wa wilaya ya Kisarawe


Rais John Magufuli amemteua aliyekuwa mshindi wa pili wa mashindano ya ulimbwende Tanzania (Miss Tanzania) 2006, kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe

Rais Magufuli ametangaza uteuzi huo leo, Julai 28 Ikulu jijini Dar es Salaam. Jokate anashika nafasi ya Happyness Senenda

Jokate alikuwa mshindi wa pili katika mashindano ya ‘Miss Tanzania’ ambapo Wema Sepetu alishinda taji hilo

Kabla ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo, Jokate alikuwa Kaimu Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM

Jokate aliteuliwa kushika nafasi hii Aprili mwaka jana na akaondolewa kwenye nafasi hiyo Machi mwaka huu
Magufuli amteua Jokate Mwegelo Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Magufuli amteua Jokate Mwegelo Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Reviewed by KUSAGANEWS on July 28, 2018 Rating: 5

No comments: