Waziri Mkuu Mh.Kassim Majaliwa amesema Serikali imeliteua
Gereza la Kwitanga lililopo wilayani Kigoma kuwa kituo kikuu cha uzalishaji wa
zao la michikichi nchini
Hivyo ameuagiza uongozi wa gereza hilo waongeze nguvu katika
uzalishaji wa michikichi kwa kupanua mashamba na kuongeza askari wenye ujuzi wa
kilimo cha michikichi na kupanda miche mipya ya michikichi na kukata ya zamani
Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati alipotembelea gereza hilo
akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi yenye lengo la kufufua zao la
michikichi mkoani Kigoma
Amesema Serikali imedhamiria kwa dhati kufufua kilimo cha
zao la michikichi mkoani Kigoma, hivyo kila mwananchi lazima awe na shamba la
michikichi
Katia hatua nyingine, Waziri Mkuu ameuagiza Mkuu wa Magereza
Mkoa wa Kigoma Bw. Sabas Matolo kuhakikisha Gereza la Kwitanga linawezeshwa kwa
kuwa na zana bora na za kisasa za kilimo yakiwemo matrekta na vifaa vya kuvunia
ili waweze kuongeza uzalishaji wa mafuta.
Pia, Waziri Mkuu amemuagiza Bw. Matolo awahamishe askari
ambao ni wataalamu wa kilimo wenye ujuzi wa zao la michikichi kutoka
kwenye Magereza mengine mkoani Kigoma na kuwahamishia katika gereza la
Kwitanga ili kuimarisha uzalishaji
Awali, Mkuu wa gereza hilo Bw. Majuto Masila alisema ili
kilimo cha michikichi na uzalishaji wa mafuta uweze kuwa na tija, wanahitaji
wafungwa wasiopungua 300 wawepo kila siku gerezani hapo ili kumudu shughuli za
shamba hilo. Kwa sasa kuna wafungwa 112
"Uzalishaji wa mafuta kwa miaka mitatu mfululizo
gerezani Kwitanga ni kama ifuatavyo mwaka 2015/2016 tulizalisha lita 16,094,
mwaka 2016/2017 lita 12,674, na mwaka 2017/2018 tulizalisha lita 16,000,"
alisema
Alisema mafuta yanayozalishwa gerezani hapo yanatumika
katika kulisha wafungwa wa gereza hilo la Kwitanga, Bangwe, Kasulu, na Kibondo.
Ziada ya mafuta hutumika kulisha wafungwa magereza ya mikoa ya Kagera, Mwanza,
Shinyanga, Singida, Dodoma, Morogoro na Tabora
Baada ya kutoka katika Gereza la Kwitanga, Waziri Mkuu
alitembea shamba darasa na eneo la kuzalisha miche ya michikichi la Seed Change
katika eneo la Mungonya na kuziagiza halmashauri zote zinazolima michikichi
mkoani Kigoma kwenda kununua mbegu kwenye shamba hilo
Gereza la Kwitanga Kuwa Chuo Kikuu cha Michikichi"Majaliwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 29, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 29, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment