Migogoro ya Kifamilia na Changamoto za Kimaisha vyapelekea kuongezeka kwa Watoto Wenye Uhitaji


Wanandoa wametakiwa kuepuka migogoro ya kifamilia ambayo ndiyo inawathiri watoto wao na kupelekea kukimbia majumbani makwao na Kwenda mitaani kisha kulelewa kama watoto wenye Uhitaji.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kundi la Friends Of Batuli Bwana Yesaya Mkwaju wakati walipotembea kutoa msaada kituo cha watoto wenye uhitaji Cha Kindness Children Care Orphanage Cente ambacho kinalea watoto wenye uhitaji kilichopo Eneo la Kijenge kata ya Mushono halmashauri ya Jiji la Arusha.

Mkwaju amesema kuwa tangu kuanza mwaka huu wa 2018 wameshatembelea vituo vitatu na kutoa misaada Mbalimbali wao kama kauli mbiu yao inavyosema  Saidia Jamii yako Kadri Ulivyobarikiwa huku akiwataka watu mbalimbali kuendelea kujitokeza kusaidia watoto wenye uhitaji.

Kwa upande wa afisa ustawi wa jamii kutoka jiji la Arusha Bi Nivoneia Kikaho ambaye aliongozana na Kundi Hilo la Friends Of Batuli kwenda kutoa misaada katika kituo hicho cha Kindness amesema kuwa mifarakano ya Ndoa pamoja na Ugonjwa wa Ukimwi imekuwa sababu ya Kuongezeka kwa watoto wenye Uhitaji.

Naye Mlezi wa Kituo Hicho ambaye ni Mkurugenzi wa Kituo Hicho cha Kindnes Children care Mchunaji Yohana Mwampamba amesema kuwa wanaume kukwepa majukumu yao katika familia na kuwaachia wanawake peke yao Pia imepelekea kuwepo kwa watoto wenye mahitaji

Hata hivyo Kundi la Friends Of batuli limekuwa na Desturi ya kutoa misaada mbalimbali kwa jamii yenye uhitaji ambapo leo katika kito hicho wametoa vyakula kwa ajili ya kusaidia watoto hao.
Migogoro ya Kifamilia na Changamoto za Kimaisha vyapelekea kuongezeka kwa Watoto Wenye Uhitaji Migogoro ya Kifamilia na Changamoto za Kimaisha vyapelekea kuongezeka kwa Watoto Wenye Uhitaji Reviewed by KUSAGANEWS on July 29, 2018 Rating: 5

No comments: