Mbunge wa jimbo la Ngorongoro ambaye pia ni naibu waziri wa
elimu sayansi na Teknolojia Mh Wiliam Olenasha amesema mpaka Kufikia mwaka 2019
vijiji 35 vitakuwa vimepata umeme katika mpango wa vijijini REA Awamu ya tatu
na baadae wataendelea na maeneo mengine.
Olenasha ameyasema hayo tar 8 August 2018 katika kijiji
cha Sakala wakati alipofanya mkutano wa hadhara wa wananchi ambapo amebainisha
kuwa kila nyumba lazima itawaka umeme kinachotakiwa ni wananchi kuwa tayari
kuupokea umeme huo.
Mbunge Olenasha amesema tayari nguzo za umeme
zinaendelea kupita katika maeneo mbalimbali lengo ni kuhakikisha ngorongoro
inabadilika kuanzia miundombinu iliyopo mpaka mazingira yenyewe ya maisha ya
watu na kuwa ngorongoro mpya.
“Wote ni mashahidi hili hatuzungumzi tena siyo hadithi nguzo
tayari zinasambaa katika vijiji tunategemea ifikapo mwaka 2019 vijiji 35
vitakua vinawaka umeme”Alisema Olenasha
Kufuatia ujio huo wa umeme wa REA Mh Olenasha amewataka
wananchi sasa kuendelea kujenga nyumba zenye ubora zaidi ili na mazingira yabadilike
kwa kuwa Ngorongoro iliyokuwa inajulikana mwanzo kwa migogoro sasa inajulikana
kwa maendeleo chanya.
Wakitoa maoni yao baadhi ya wananchi wamesema kuwa ujio
wa umeme utawarahisishia sana wao kufanya maendeleo ikiwemo kukuza kipato kwa
wafanyabiashara ambao wanategemea umeme tofauti na ilivyo hivi sasa wanapata
changamoto ya huduma ya matumizi ya vitu vinavyohitaji umeme.
Katika ziara hiyo ya Mbunge kutembelea wananchi wa jimbo
lake wengi wa wadau wa maendeleo pamoja na wananchi wamempongeza Olenasha kwa
kuendelea kutekeleza ahadi zake alizoahidi kipindi alipoomba kura ya
kuchaguliwa kuwa Mbunge wa jimbo hilo la Ngorongoro.
Jimbo la Ngorongoro lenye kata 28 Olenasha
ameshatembelea zote na kuzungumza na wananchi ambapo hii ni mara ya nne kufanya
hivyo jambo ambalo wabunge wengi wamekuwa hawafanyi hivyo kufanya muendelea
kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi waliowachagua.
Ngorongoro wapata Umeme wa REA tatu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 08, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment