Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemtaka Balozi wa Marekani afikishe salamu zake kwenye Kampuni ya ndege ya Boeing kuwa wakamilishe haraka ndege ya pili inayotakiwa kufika Tanzania kwa kuwa hela za kulipia zipo.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, wakati wa sherehe za kupokea ndege mpya ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyowasili leo kutokea Seattle nchini Marekani.
"Ndege hizi ni matokeo ya
Watanzania kulipa kodi na kuchapakazi. Nawapongeza wote walioshiriki
kikamilifu. Ndege zote hizi tumenunua kwa fedha zetu wenyewe, hatujakopa
kwa mtu. Tunataka Balozi wa Marekani utufikishie salam Boeing kuwa ile
Dreamliner ya pili waikamilishe haraka, hela tunazo" - Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli ameongeza kwamba "Madai
kuwa Watanzania wengi hawafaidiki na ndege hayana msingi. Wapo wengi
wanaohitaji ndege bei ilikuwa juu. Ndege hii imewafurahisha wengi na
kama yupo mtu hajafurahia tukio hili basi huyo atapata tabu sana!-Rais Magufuli
Pamoja na hayo Rais amefafanua kuwa
ndege hiyo imeletwa ili iweze kuimarisha na kuongeza mapato ya utalii
nchini kwa kuwa 70% ya watalii wanatumia ndege.
Mh. Rais amesisitiza kwamba "Ukiongeza
ndege wasafiri wanaongezeka. ATCL imeongeza wasafiri kutoka 4000 kwa
mwezi mpaka 21,000 kwa mwezi. Tunaboresha usafiri wa reli, majini na
barabara. Waliodhani kuwa maboresho ya Bandari hayana tija sasa
wameaibika".
"Hela tunazo" - Rais Magufuli
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 08, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 08, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment