Waziri wa Maliasili na
Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, amewasimamisha kazi Maofisa na Askari
Wanyamapori wote 27 wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania,
TAWA ,katika Pori la Akiba Uwanda akiwemo Kaimu Meneja, Lackson Mwamezi
kwa kushindwa kusimamia vizuri pori hilo.
Hatua
hiyo imekuja ikiwa ni siku tatu tangu amsimamishe kazi Meneja wa Pori
hilo, Mark Chuwa kwa tuhuma kama hizo pamoja na tuhuma nyingine ikiwemo
kushindwa kuondoa ngo'mbe zaidi ya 12,000 ambao wamedaiwa kuwepo ndani
ya pori hilo.
Amefafanua kwamba, tuhuma hizo kuwa ni
pamoja na kudaiwa kujihusisha na vitendo vya kuomba na kupokea rushwa
kutoka kwa wavuvi wanaovua samaki Ziwa Rukwa kwa kuwatoza kila mmoja
Shilingi 100,000 kwa mwezi na kuruhusu mifugo kuchungwa hifadhini kwa
kipindi cha miezi mitatu ambapo kila mfugaji hutozwa kati ya Shilingi
milioni sita hadi saba.
Wakati huo huo, Dk. Kigwangalla ametoa
siku 30 kwa wananchi wote wenye mifugo ndani ya pori hilo kuitoa kwa
hiari yao wenyewe kabla ya operesheni maalum itakayowaondoa kwa nguvu.
Pori la Akiba Uwanda lipo katika Bonde
la Ziwa Rukwa katika Wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa na linasimamiwa
na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, TAWA.
Kigwangalla atumbua Askari 27
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 08, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 08, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment