Rais John
Magufuli amebainisha sababu za kununua ndege ikiwa ni pamoja na kujenga heshima
na kulinda hadhi ya Taifa.
Amesema
ilikuwa aibu kwa Tanzania, nchi yenye idadi ya watu zaidi milioni 50 kutokuwa
na ndege
Pia, amesema
Watanzania wengi wamefurahia ujio wa ndege hiyo na kwamba, kama wapo ambao
hawajafurahia basi watapata tabu sana
Dk Magufuli
amesema hayo leo Julai 8, 2018 akipokea ndege aina ya Boeing 787- 8 Dreamliner
iliyowasili saa 11:15 jioni
Amesema
ununuzi wa ndege hiyo ni jitihada za Watanzania wote ambao wanalipa kodi
Rais ametaja
sababu nyingine kuwa ni kuboresha huduma ya usafiri wa ndege nchini kwa sababu
Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) lilikuwa na ndege moja pekee yenye uwezo wa
kubeba abiria 51
Amesema
Watanzania wengi hawatumii usafiri wa ndege lakini haimaanishi kwamba hawapendi
kutumia aina hiyo ya usafiri
“Hawatumii kwa
sababu ndege zilikuwa zinakwenda miji mitatu pekee, lakini sasa wanatua kwenye
miji 12," amesema Rais Magufuli
Amesema pia
gharama zilikuwa kubwa, hivyo ujio wa ndege hiyo utapunguza gharama za usafiri
na wananchi wa kawaida wataweza kusafiri
Rais Magufuli
amesema sababu nyingine ni kukuza sekta ya utalii nchini
"Tunataka
tuwe tunafanya safari za kimataifa. Ninaamini tukianza na ndege hii na ile
nyingine ikija, ni wazi kwamba idadi ya watalii nchini itaongezeka,"
amesema
Katibu Mkuu
Kiongozi, Balozi John Kijazi amesema ununuzi wa ndege una manufaa makubwa
ambayo ni pamoja na kuimarisha mtandao wa usafiri nchini
"Ndege
hizi zitaimarisha biashara, uwekezaji na utalii nchi. ATCL zitunzeni ndege na
muweke mipango mizuri ya biashara na kuilipa serikali fedha za ukodishaji kwa
mujibu wa mkataba," amesema Balozi Kijazi
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Leonard Chamliho amesema ndege ya
Dreamliner itaanza safari katika miji ya Dar es Salaam, Kilimanjaro na Mwanza
ili kuwapa uzoefu marubani
Amesema
Septemba, 2018 ndege hiyo itaanza kwenda Bombay (India), Bangkok (Thailand) na
Guangzhou (China
Pia, amesema
wameanza mchakato ili ndege hiyo iwe inatua Uingereza.
Rais Magufuli ataja sababu za kununua ndege
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 08, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 08, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment