Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA),
imekanusha taarifa zinasombazwa kupitia mitandao ya kijamii zilizodai kuwa
mtandao wa ‘whatsapp’ utaanza kulipiwa kuanzia Julai 10, mwaka huu.
Kupitia taarifa iliyotolewa na
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Mamlaka ya Mapato (TRA), Richard
Kayombo imesema kuwa taarifa hizo zinazodai kuwa mtandao huo utaanza kulipiwa
kiasi cha shilingi elfu 15 kuanzia Julai 10 hazina ukweli wowote.
“Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA),
inapenda kuufahamisha Umma kuwa, taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya
kijamii zikidai kwamba Mtanzania yeyote anayetumia whatsapp atatakiwa kulipia
shilingi 15,000/= kuanzia tarehe 10 mwezi huu ni za uongo”, imesema taarifa.
Mamlaka hiyo imetoa wito kwa
watumiaji wa mtandao ya kijamii kuwa makini na kupuuza taarifa hizo kwakuwa
hazina ukweli wowote.
TRA yafunguka kuhusu kulipia ‘Whatsapp’
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 03, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 03, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment