Ongezeko la watu ni mzigo wa serikali


Imeelezwa kuwa kasi ya ongezeko la Watu Nchini, ni mzigo kwa serikali kwani ndiyo chanzo cha kuibuka kwa changamoto nyingi katika sekta za jamii, ikiwemo Afya, Elimu na miundombinu. 
 
Hayo yamesemwa na Afisa uhusiano na mawasiliano, kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani (UNFPA), Warren Bright  wakati akizungumza amebainisha kuwa kasi ya ongezeko la watu ni kubwa na haiendani na kasi ya maendeleo ya kijamii na kupelekea changamoto kuwa kubwa, kwa kuibebesha mzigo mkubwa serikali.

“Matumizi ya uzazi wa mpango imekuwa ni changamoto kubwa, kuna ongezeko kubwa sana la idadi ya watu na kuna athari zipo na zitaendelea kuwepo kama jamii haitakubaliana na mabadiliko ya tabia ya nchi na mazingira Duniani”, amesema Warren.

Ameongeza kuwa, “ongezeko la watu Zanzibar kwa sasa limekuwa mara mbili zaidi, hivyo serikali bado itabebeshwa mzigo tu hata ikitoa huduma za jamii bure, hatuwezi kuhudumiwa wote”.

Wakati Dunia ikielekea kuadhimisha siku ya idadi ya watu duniani, Julai 11, Ripoti ya makadirio ya watu nchini iliyozinduliwa Februari 28, 2018, na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango inaonyesha Tanzania kuna idadi ya watu 54.2 milioni hadi kufikia mwaka 2018 huku ikieleza kuwa kila mwaka kuna ongezeko la watu milioni 1.6.

Ongezeko la watu ni mzigo wa serikali Ongezeko la watu ni mzigo wa serikali Reviewed by KUSAGANEWS on July 03, 2018 Rating: 5

No comments: