Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya
Handeni wametishia kumchukulia hatua Mkurugenzi wa halmashauri hiyo kutokana na
kupata hati yenye mashaka.
Hayo yamejiri wakati wa kikao maalum
cha kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali kwa
mwaka wa fedha 2016 hadi 2017 ambapo halmashauri ya wilaya ya Handeni
imepata hati yenye mashaka jambo lililoacha baadhi ya madiwani kutokuwa na
imani na mkurugenzi wao.
Hata
hivyo mkurugenzi katika kuhakikisha hapotezi kibarua chake amesema kuwa kuanzia
sasa ataanza kuchukua hatua kwa wakuu wa idara waliohusika na upatikanaji wa
hati hiyo inayotia mashaka.
Kikao
hicho ambacho kimehudhuriwa na mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shighela nae
akawaunga mkono madiwani hao kwa kusema kuwa wasiwaonee haya watumishi ambao
wamekuwa chanzo cha halmashauri hiyo kupata hati chafu.
Madiwani wageuka 'mbogo' mbele ya Mkurugenzi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 03, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 03, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment