Shirikisho la soka Hispania, limemshukuru aliyekua Kocha wa
muda wa timu ya Taifa, Fernando Hierro aliyejizulu wadhifa huo juzi, akisema
anawajibika kwa kushindwa kuipa mafanikio katika fainali za mwaka huu za
Kombe la Dunia
Hierro alipewa jukumu hilo siku mbili kabla ya kuanza
harakati za kusaka taji la fainali za Kombe la Dunia 2018, akichukua nafasi ya
Julen Lopetegui, aliyetimuliwa na Shirikisho hilo akiwa Russia, baada ya
kukubali kuteuliwa kuwa Kocha wa Real Madrid
Hata hivyo kuondoka Lopetegui kumeonekana kuwa pigo kuliko
namna Shirikisho hilo lilivyodhani kwani Hierro, hakuweza kuivusha Hispania
hata 16 bora
Hilo lilikua pigo kwa mabingwa hao wa Dunia mwaka 2010 ambao
hawakuonyesha soka la kuvutia katika fainali za mwaka huu kiasi cha kubezwa
Hierro, mwenye miaka 50, amekataa pia kurudi katika nafasi
yake ya awali ya Mkurugenzi wa Ufundi akisema anafikiria jambo jingine la
kufanya.
Shirikisho la soka
Hispania limelaumiwa sana kwa kumuondoa Lopetegui ambaye tangu ateuliwe kushika
wadhifa huo mwaka 2016 baada ya kustaafu kwa Vicente del Bosque, alikuwa
hajashindwa hata mechi moja
Sijatenda haki najiuzulu – Hierro
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 09, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 09, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment