Baada ya gari la abiria linalofanya
safari zake Arusha - Dar es salaam kuteketea kwa moto maeneo ya Tegeta,
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda Maalum ya Dar es Salaam,
Marison Mwakyoma amesema bado wanamsaka dereva wa basi hilo ili kuweza kutoa
maelezo ya kina juu ya ajali hiyo.
Akizungumza
Kamanda Mwakyoma amesema kwamba ingawa taarifa za awali zinadai kwamba ni
kufeli kwa breki ya nyuma, lakini zipo sababu za msingi ambazo zinaweza
kutolewa na dereva huyo kwani tukio lililopelekea gari hilo kulipuka halikuwa
la ghafla.
Akizungumzia ajali hiyo iliyotokea
Tegeta jana usiku, Kamanda Mwakyoma amesema kwamba basi hilo lilitokea Arusha
likuwa na abiria 42, ambapo 22 walishukia Bagamoyo na wengine waliosalia
walifikia maamuzi ya kushuka
baada ya kuona gari linazidi kutoa harufu na ndipo dereva alipoamua kulitelekeza.
baada ya kuona gari linazidi kutoa harufu na ndipo dereva alipoamua kulitelekeza.
Aidha Mwakyoma ameongeza kwamba siyo
kila ajali husababishwa na uzembe wa dereva kwani yapo mambo mengi ikiwepo
nyaya za umeme kugusana, ku-jam kwa breki ya gari hivyo wamiliki wa magari
wanapaswa kuwa makini wanapofanya 'service' ya magari ikiwa ni pamoja na
kutazama mfumo mzima wa umeme na siyo kumwaga 'oil'.
Pamoja na hayo Mwakyoma amesema
uchunguzi wa kina wa kuhusu ajali hiyo bado unaendelea kufanyika na sasa
wanasubiria hati ya ukaguzi wa gari hilo kutokea Arusha kabla ya safari.
Dereva wa basi lililowaka moto asakwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 09, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 09, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment