Serikali kupitia Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imewataka wananchi kutoa taarifa
kwa hospitali, zahanati au kituo cha afya chochote kitakachokuwa kinatoa majibu
ya kipimo cha typhoid ndani ya nusu saa kwa kuwa siyo utaratibu za kitabibu.
Tamko hilo limetolewa na Naibu wa
Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Faustine Ndugulile wakati akizungumza na eatv.tv leo
Julai 10, 2018 baada ya kupita siku kadhaa tokea alivyotoa kauli yake iliyozua
taharuki na kuwaacha wengi njia panda kuwa 'asilimia 70 ya homa Tanzania siyo
malaria wala siyo typhoid, hivyo unapokwenda kwenye vituo vya afya kupimwa
halafu ukaambiwa una typhoid inabidi uhoji ni kigezo gani kilichotumika mpaka
uambiwe unaumwa ugonjwa huo'.
"Mara nyingi sana katika vituo
vyetu vya kutoa huduma ya afya kumekuwa na tatizo la kila mgonjwa kuwa na
malaria au muda mwingine kusema ana typhoid. Utaratibu wa kupima kipimo cha
Typhoid sio kama wanavyosema kuwa unaenda leo unapimwa halafu unapatiwa majibu
ndani ya nusu saa. Mara nyingi kipimo hiki huwa kinatoa majibu ndani ya saa
48", amesema Dkt.Ndugulile.
Pamoja na hayo, Dkt. Ndugulile
ameendelea kwa kusema "siasa na afya ni vitu viwili tofauti hivyo
nawaomba wananchi wasipuuzie suala hili la kuhoji endapo watapewa majibu ya
typhoid ndani ya nusu saa maana hiyo ni haki yao ya msingi".
Kwa upande mwingine, Naibu wa Waziri
Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa mtu yoyote ambaye atalalamika kutopewa
haki za msingi anapokuwa amekwenda hospitalini, anayohaki ya kwenda kufungua
mashitaka na mtoa huduma kuchukuliwa hatua stahiki.
Serikali yawapa angalizo wananchi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 11, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 11, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment