Naibu waziri wa elimu sayansi na Teknolojia Mheshimiwa
William Olenasha Ameagiza kukamatwa kwa mwalimu wa Shule ya Sekondari Loliondo
Erick Kalaliche kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wake wa kidato cha tatu (jina
limehifadhiwa)ambaye kwasasa amehamia mkoa wa Lindi baada ya Kutenda Kosa Hilo.
Akizungumza katika kikao cha dharura kilichofanyika
katika makao makuu ya halmashauri ya Ngorongoro Mheshimiwa Olenasha amesema
kwamba jambo hilo linasikitisha na kuidhalilisha sekta ya Elimu na lazima hatua
za kisheria na Kinidhamu zichukuliwe mara moja.
Amesema wizara ya Elimu haiwezi kuvumilia walimu ambao
wanafundisha watoto ambao pia ni kama wazazi wanaofumbia macho vitendo vya
vichafu ambavyo vinarudisha nyuma sekta ya Elimu na juhudi za serikali ya kuhakikisha
watoto wanapata elimu Bora.
Afisa elimu wa wilaya ya Ngorongoro Bwana Emanuel Sukums
amekiri mwalimu huyo kutenda kosa la kumbaka mwanafunzi huyo ambapo kitendo
hicho kilifanyika mwezi wa tatu na kujulikana mwezi wa sita ambapo hakuna hatua
zozote za kinidhamu zilizochukuliwa.
Amesema kuwa mwalimu Erick alimchukua mwanafunzi huyo
ambaye alikuwa anasoma kidato cha tatu katika shule hiyo ya Sekondari Loliondo na
kumpeleka nyumba ya kulala wageni na kumbaka.
Tarehe 9 July 2018 naibu waziri wa Elimu sayansi na
Teknolojia Mh William Olenasha alifanya ziara ya Kushtukiza shule ya sekondari
Loliondo na kuhoji kuhusiana taarifa za mwalimu huyo ambapo mwalimu mkuu wa
Shule hiyo Bi Neema Mchao alikosa majibu sahihi mbele ya Naibu waziri lakini
baadae kukiri kwamba mwalimu alihama shuleni na alikuwa ametenda kosa hilo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Loliondo Bi Neema
Mchao amekiri kufuatilia jambo hilo lakini alipohojiwa kwanini hakuchukua hatua
za kinidhamu alisema yeye aliachia mamlaka husika kwasababu hata yeye jambo
hilo lilimsikitisha.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye ni mkuu
wa wilaya ya Ngorongoro Rashidi Mfaume Taka amesema kuwa utaratibu unafanyika kurudishwa
kwa mwalimu huyo kutoka mkoa aliyohamishiwa kuja Ngorongoro kwa kuwa kitendo
alichokifanya ni Udhalilishaji katika wilaya hiyo.
Kufuatia kikao hicho mkuu wa Polisi wilayani Ngorongoro
amemtaka Mkuu wa Shule ya Sekondari Loliondo pamoja na Afisa Elimu kufika
kituoni kwa ajili ya Uchunguzi zaidi wa
tukio hilo.
Naibu Waziri Wa Elimu aagiza kukamatwa mwalimu aliyebaka mwanafunzi wa kidato cha tatu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 10, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment