"Nilipochaguliwa na wananchi wa Ngorongoro Niliahidi Maji,Barabara,Afya na Elimu wenyewe Mnaona "Mbunge Olenasha


Mbunge wa jimbo la Ngorongoro amesema maendeleo ambayo yanakuja kwa kasi pamoja na miradi mikubwa ya maendeleo ni kwasababu ya ushirikiano wake na wananchi waliomchagua kuwawakilisha Bungeni.

Akizungumza katika ziara yake ya Jimbo kutembelea wananchi wake na kuwaeleza mafanikio yaliopatikana kwa miaka miwili tangu alipochaguliwa na wananchi wake Olenasha amesema wananchi wamekuwa mstari wa mbele katika kuleta maendeleo ambayo kwasasa yanaonekana

Olenasha amesema alipochaguliwa na wananchi aliapa kuhakikisha maendeleo ya maji,barabara ya lami,Afya,Umeme pamoja na elimu bora yanaenda kwa wananchi waliompigia kura awe muwakilishi wao kitu ambacho ametekeleza na sasa miradi inaendelea kujengwa.

Amesema yeye kama Mbunge hapendi kuona wananchi wake wanateseka wakati yeye yupo na anauwezo wa kutekeleza aliyoyaahidi siku ambapo alisimama jukwaani kunadi sera ambazo zimempa yeye kuwa mbunge.

“Wananchi wangu mimi mmenichagua nisumbueni nitumeni ndiyo mana nimerudi kwenu mimi siyo Mbunge wa kupotea potea na mpaka sasa hivi nyie wananchi wangu ni mashahidi tangu nimekuwa muwakilishi wenu nimepita kila kata mara nne na sasa nimerudi tena na nitaendelea kuja na sitawachoka”Alisema Olenasha

Olenasha ameongeza kuwa kila akitembea anawaza maendeleo ya wananchi wake waliomchagua ambao wamempa mzigo wa kuwatumikia chini ya serikali ya Awamu ya Tano ya Raisi Dokta John Pombe Magufuli ya hapa Kazi tu.

Hata hivyo amesema yuko tayari kurudi katika jimbo lake mara kwa mara kwa ajili ya wananchi licha ya kuwa na majukumu mengi ya kiserikali atarudi kila wakti kwa ajili ya kushirikiana na wananchi kusimamia miradi mikubwa ya maendeleo iliyopo

Akizungumza mmoja wa mwanachi katika kata ya Samunge Bwana Modeli Kibwana amesema kuwa kwasasa mbunge waliyempata amewaletea maendeleo kuliko kipindi chochote kile cha viongozi waliopita

Amesema Mbunge Olenasha amekuwa mstari wa mbele kusimamia miradi anayoileta na wanaishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kushirikiana na Mbunge wao kufanya mambo yaliyoshangaza kila mtu aliyekua anaijua Ngorongoro kwa migogoro.

Naye Jumanne Bwanga amesema kwamba hawatarajii kuona mtu anawatoa kwenye mstari wa maendeleo na wao kama wananchi watahakikisha miradi inayoletwa kupitia Mbunge wao wataisimamia kwa nguvu zote bila kuhujumiwa.



"Nilipochaguliwa na wananchi wa Ngorongoro Niliahidi Maji,Barabara,Afya na Elimu wenyewe Mnaona "Mbunge Olenasha "Nilipochaguliwa na wananchi wa Ngorongoro Niliahidi Maji,Barabara,Afya na Elimu wenyewe Mnaona  "Mbunge Olenasha Reviewed by KUSAGANEWS on July 11, 2018 Rating: 5

No comments: