Wakati taasisi ya TWAWEZA
ikipewa siku saba kujieleza ni kwanini isichukuliwe hatua za kisheria
kwa kutoa matokeo ya utafiti bila ruhusa Tume ya Sayansi na Teknolojia
(COSTECH), imesema kuwa imesikitishwa na kusambaa kwa barua hiyo
mtandaoni.
Mara
baada ya kusambaa kwa barua ya TWAWEZA iliyoandikwa kutokea COSTECH,
Kaimu Mkurugenzi wa tume hiyo Dkt. Amos Nungu amesema kuwa baada ya
kufuatilia barua hiyo waligundua kuwa ni yao.
“Baadaya
kufanya uchunguzi tuligundua kuwa barua inayosambaa mitandaoni ni yetu
tulioiandika kwenda TWAWEZA, tunasikitika kuona mawasiliano halali ya
kiofisi yanapelekwa mitandaoni hata kabla ya kujibiwa”, amesema Dkt. Nungu.
Dkt.
Nungu amesema kuwa COSTECH pekee ndio chombo cha kutoa ushauri katika
masuala yote yanayohusu sayansi, teknolojia na uvumbuzi na moja ya
majukumu yake ni kusajili na kutoa vibali vya tafiti zote za muda mfupi
na mrefu zinazofanywa nchini.
Mwishoni
mwa wiki iliyopita TWAWEZA ilitoa ripoti ya utafiti wa sauti za
wananchi ukieleza hali ya siasa nchini, ambapo utafiti ulionesha
kuporomoka kwa ukaribu wa wananchi na viongozi wa vyama vya siasa.
COSTECH yasikitishwa na uamuzi wa TWAWEZA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 12, 2018
Rating: 5
No comments:
Post a Comment