Jeshi la Polisi limefanikiwa
kumkamata mwalimu wa shule ya sekondari Loliondo, Erick Kalaliche mkoani
Lindi ambaye anatuhumiwa kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wake wa kidato
cha tatu (jina limehifadhiwa)katika shule ya sekondari Loliondo kabla ya mwalimu huyo
kuhamishwa.
Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng'anzi wakati akizungumza na KUSAGANEWS baada
ya Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha
kutoa agizo la kutafutwa na kukamatwa kwa mwalimu huyo ambaye ametenda
kosa la jinai na kuhamia katika shule nyingine.
"Agizo la Naibu Waziri wa Elimu tumelipokea na kama
inavyofahamika kuwa kumpa ujauzito mwanafunzi ni kosa la jinai na jarada
limeshafunguliwa la kupeleleza tukio hilo kwasababu baada ya
kuwasiliana na Mkurugenzi wake yule
mwalimu alipewa uhamisho tangu mwaka 2017 lakini tumewasiliana na
wenzetu katika kituo chake kipya kule Lindi na wametuambia kwamba
wamefanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo leo hivyo tunafanya mpango wa
kurudishwa huku kwenye kesi yake", amesema Kamanda Ng'anzi.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Elimu William Ole-Nasha amesisitiza
kuwa, Wizara yake haiwezi kuvumilia walimu wanaofundisha watoto ambao
pia ni kama wazazi wanaofumbia macho vitendo vichafu ambavyo vinarudisha
nyuma sekta ya elimu na juhudi za serikali za kuhakikisha watoto wa
kike haki yao ya elimu.
Jeshi la Polisi lamdaka mwalimu aliyebaka
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 13, 2018
Rating: 5
No comments:
Post a Comment