Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole ametoa
sababu za mkutano wa kumkaribisha aliyekuwa mbunge wa Monduli (Chadema), Julius
Kalanga kufanyika usiku
Akizungumza Polepole amesema mkutano huo umefanyika jana
usiku kwa kuwa ndio muda pekee uliopatikana kutokana na kutingwa na shughuli
nyingi
Polepole na Kalanga kwa pamoja, walizungumza na Watanzania
usiku wa kuamkia leo kupitia kurasa za mtandao wa kijamii za facebook na
Twitter za katibu huyo wa itikadi na uenezi
Katika mazungumzo hayo, Kalanga alitangaza kujivua uanachama
wa Chadema na kujiunga na CCM, usiku huohuo
Unajua jana nilikuwa Tarime (Mara), nikaenda Mwanza pale
nilikuwa na kikao, kisha nikaenda Dar es Salaam ambako nilikuwa na
shughuli. Baadaye nilikwenda Kilimanjaro na Arusha. Nilifanya mkutano
jana usiku kwa kuwa ndio muda niliokuwa nao,” amesema Polepole
“Ingawa ilikuwa usiku lakini mazungumzo yale yamefuatiliwa
na watu wengi kweli kweli na wengi walipiga simu hadi kutoka nje ya nchi.”
Amesema kuna wabunge zaidi wa Chadema wanatamani kujiunga na
CCM
“Kuna wabunge ambao tumeweka msimamo kama chama kwamba
hatuwezi kuwapokea hata wakitaka. Huwezi kuwa na mbunge yeye kazi yake ni kuota
ndoto tu,” amesema
Sababu Polepole, Kalanga kukutana usiku hii hapa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 31, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 31, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment