Ridhiwani atoa neno wimbi la wapinzani kujiunga CCM


Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete amesema sababu ya wapinzani kuhamia chama tawala inatokana na mambo mazuri yanayofanywa Serikali ya Awamu ya Tano

Ametoa kauli hiyo leo Jumanne Julai 31, 2018 kupitia ukurasa zake za mitandao ya kijamii

Amesema kutokana na wimbi hilo la wapinzani kuhamia CCM wa kulaumiwa ni Serikali hiyo kutokana na kufanya mambo ya uhakika yanayowavutia

Wabunge wengine wa Chadema waliotimkia CCM ni Mwita Waitara na Dk Godwin Mollel. Dk Mollel alipitishw ana CCM kuwania tena ubunge katika jimbo la Siha na kuibuka mshindi

Kupitia ukurasa wake Ridhiwani amesema, “kama hauwezi pambana ungana nasi karibuni nyumbani kumenoga.”
Ridhiwani atoa neno wimbi la wapinzani kujiunga CCM Ridhiwani atoa neno wimbi la wapinzani kujiunga CCM Reviewed by KUSAGANEWS on July 31, 2018 Rating: 5

No comments: