Serikali imezindua mkakati wa kupambana na biashara haramu ya binadamu, huku Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola akisema watapita nyumba kwa nyumba kubaini wanaotumikishwa wakiwamo wasichana wa kazi za ndani

Kwa mujibu wa Umoja wa Mtaifa, Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye tatizo la usafirishaji wa binadamu.

 Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya kupinga biashara haramu ya usafirishaji binadamu, Lugola alisema si rahisi kufikia maendeleo yanayotajwa ikiwa biashara hiyo ndani ya nchi itaachwa. “Hatuwezi kuendelea kuwa na kundi la watu linalojihusisha na usafirishaji wa binadamu, hii ni sawa na utumwa,” alisema

Alisema watu wengi wakiwamo watoto wanaotumbukia kwenye biashara hiyo hudanganywa kupewa kazi lakini wakifika maeneo husika, hukutana na kazi nje ya makubaliano yao

Lugola alisema wapo waajiri wanaotumia nguvu ya fedha na sheria za kazi kama kichaka cha kuwatumikisha wengine ambao wakibainika watashughulikiwa

Kuhusu biashara haramu ya binadamu kwa Watanzania wanaotumikishwa nje ya nchi, Lugola alisema wengi wao hudanganywa kwa mishahara mikubwa na kazi zenye staha tofauti na hali wanayoikuta huko.</p></div><div><p>Alisema zaidi ya Watanzania 22, nje ya nchi wamejisalimisha kwa kutoa taarifa za kutumikishwa

Naye mwenyekiti wa Kamati ya Kudhibiti Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu, Abeatus Magere alisema kati ya mwaka 2015 na 2018 watu 327 wameokolewa kutoka biashara hiyo

Alisema kati yao, watu 45 ni wageni kutoka nje ya nchi

“Tangu mwaka 2015 hadi mwaka huu kesi 24 zimefikishwa mahakamani na saba kati yake, wamepatikana na hatia,” alieleza

Magere alisema uzoefu wao unaonyesha kuwa vita hiyo ni ngumu na inaweza kuhatarisha maisha kwa wale wanaopambana kuidhibiti

Mratibu wa mradi kutoka Shirika la Utetezi wa Haki za Watoto na Wanawake (Kiwohede), Eda Kawala alisema Serikali haina budi kufanya uchunguzi wa kina kujua ukubwa wa tatizo la usafirishaji wa binadamu nje ya nchi

Alisema kituo chao kwa sasa kina watoto wawili wa biashara hiyo ndani ya nchi na wengine kumi waliofanyiwa ukatili mbalimbali

Kawala alisema mwaka jana walimuokoa mtoto wa miaka 13 aliyekuwa anatumikishwa japo alipopimwa alikuwa mjamzito na tayari alikuwa ameambukiwa magonjwa ya zinaa vikiwemo virusi vya Ukimwi

Alishauri Serikali kuandaa sheria itakayowabana wasafirishaji na wale wanaofanikisha mpango wa biashara hiyo

Reviewed by KUSAGANEWS on July 30, 2018 Rating: 5

No comments: