Raisi Dkt Magufuli abadilisha historia ya Wilaya ya Ngorongoro iliyokuwa inatambulika kwa Migogoro ya Ardhi


Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro ambaye pia ni naibu waziri wa Elimu sayansi na Teknolojia Mh William Tate Olenasha amempongeza raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli Kwa kupeleka mradi wa kihistoria wa ujenzi wa barabara ya lami Kilomita 213 kutoka Loliondo mpaka Mto wa Mbu ambao Mpaka kukamilika kwake utagarimu kiasi cha Shilingi Bilioni 87.

Olenasha ametoa pongezi hizo wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Pinyinyi kwenye mkutano wa hadhara katika ziara ya kuwatembelea wananchi wa jimbo lake ili kuwaeleza mafanikio tangu amechaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo hilo.

Amesema kuwa mradi huo ni wa kihistoria ambao haujawahi kutokea tangu kipindi cha kupatikana kwa uhuru na endapo barabara hiyo itakamilika utarahisisha kukuza uchumi wa wilaya ya Ngorongoro kukua kwa kasi.

Ameongeza kuwa siyo rahisi kupata pesa hizo shilingi Bilioni 87 kwa kuwa walipita wabunge wengi katika nafasi hiyo lakini serikali kupitia awamu ya tano ya Raisi Magufuli imebadilisha historia ambayo kwa muda mrefu baadhi ya watu walijua ni jambo ambalo halitawezekana lakini sasa ujenzi umeanza.

Mbunge Olenasha amesema kuwa kwa mara ya kwanza ngorongoro inaingia kwenye ramani ya Tanzania ambapo mradi huo unatekelezwa kwa vitendo na tayari ujenzi umeshaanza na kwa histori pia hawajawahi kupata barabara ya Lami licha ya kukaa serikalini kwa muda Mrefu.

Pia ameongeza kuwa lazima amshukuru Mh Raisi kwa niaba ya wananchi wake kwa sababu haijawahi kutokea kwa kipindi chote cha serikali zilizokua madarakani.

Olenasha amesisitiza kuwa wilaya ya Ngorongoro ilikuwa ikitambulika zaidi kwa migogoro ya ardhi lakini kwasasa historia imebadilika imekuwa wilaya inayokuja kwa kasi katika suala zima la maendeleo 

Ameongeza kuwa waandishi wa habari walipokuwa wakija Ngorongoro walikuwa ni kwa ajili ya kuripoti masuala yanayohusu mvutano wa ardhi na migogoro lakini kwasasa wanafika kwa picha ya kuwepo kwa maendeleo kutokana na miradi mikubwa pamoja na kuitangaza ngorongoro ambayo imeandika historia kwenye ramani ya Nchi ya Tanzania.

Tangu uhuru jimbo la Ngorongoro halikuwahi kuwa hata na mita moja ya Lami lakini kupitia Mbunge wa Ngorongoro Mh Olenasha kwa kushirikiana na serikali ya Raisi Magufuli sasa kilomita 213 zinajengwa kwa lami ambapo historia imeandikwa




Raisi Dkt Magufuli abadilisha historia ya Wilaya ya Ngorongoro iliyokuwa inatambulika kwa Migogoro ya Ardhi Raisi Dkt Magufuli abadilisha historia ya Wilaya ya Ngorongoro iliyokuwa inatambulika kwa Migogoro ya Ardhi Reviewed by KUSAGANEWS on July 07, 2018 Rating: 5

No comments: