Magufuli amwaga Mabilioni ya Fedha Ngorongoro Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya na vituo vya afya

Wilaya ya Ngorongoro imeanza kuandika Historia kwa upande wa afya baada ya kiasi cha shilingi Bilioni 1 na milioni 500 kutengwa kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya pamoja na ujenzi wa vituo 3 vya afya vya kisasa ambavyo kila kimoja kitagarimu Shilingi Milioni 400.

Hayo yamesemwa na mbunge wa jimbo la Ngorongoro ambaye pia ni naibu waziri wa elimu sayansi na Teknoloji Mh William Olenasha wakati akizungumza na wananchi alipokuwa mgeni rasmi wa zahanati ya Neema iliyopo wilayani Humo.

Olenasha amesema kuwa Ofisi ya Raisi Tamisemi tayari chini ya Raisi Dokta Magufuli wameshatoa fedha hizo ambapo ujenzi umeshaanza na wananchi wamejitolea eneo kwa ajili ya Ujenzi ambapo kwa mara ya Kwanza wilaya hiyo inakuwa na Hospitali ya Serikali ambayo ni ya wilaya.

“Tumeingia kwenye ramani ya nchi kiafya nasisi tutakuwa na hospitali ya wilaya tunapozungumzia hospitali ya wilaya tunazungumzia kitu ambacho wote hatuna cha kufananisha nacho katika wilaya yetu kwasababu haijawahi kuwepo kwahiyo ni tayari ni uwekezaji mkubwa ambao umefanywa na serikali”Amesema Olenasha

Pia Mbunge Olenasha ameongeza kuwa katika kipindi hicho cha miaka miwili na nusu cha uongozi wake chini ya Raisi Magufuli wamepata fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vitatu vikubwa vya afya kimoja tayari ujenzi kilichoko sakala kinakamilika cha pili kitajengwa Samunge na kituo cha tatu kitajengwa eneo la Osinoni ambavyo vyote vitagarimu shilingi Milioni 400.

“Kwa hiyo wanachi wangu kama mkiangalia huo ni uwekezaji wa zaidi ya shilingi bilioni 3 ndani ya kipindi cha miaka miwili kuna huduma nyingine zinaendelea na ujenzi unaoendelea wote mnafahamu kwamba katika wilaya yetu tuna hospitali mbili ile ya enduleni lakini naya Waso ambazo zote ni za binafsi lakini pia tuna vituo 5 vya afya lakini tuna zahanati 28 ikiwemo hii hapa kwa hiyo tayari mko tayari kwenye orodha yangu kwenye vituo ambavyo tunavyo kama mnavyoona tayari tunamaendeleo lakini bado tuna nafasi kubwa ya kuboresha mazingira ya afya”Amesema Olenasha Mbunge 

Pamoja na hayo amewaomba wananchi kujiunga na bima ya afya kwasababu itakuwa rahisi kila mwananchi kupata huduma kwa bei rahisi zaidi pamoja  na kuborsha huduma za afya.

Kwa upande wa Dokta Richard Nkambi ambaye ni mmiliki wa zahanati hiyo amesema kuwa kuanzishwa kwa huduma ya afya  kutarahisisha utoaji wa huduma ambapo kabla kituo hicho hakijazinduliwa rasmi kwa mwezi uliopita zaidi ya wananchi 300 wameshapatiwa huduma ambapo matayarijio yao kwa mwezi ni kuhudumia wananchi 600.

“Zahanati hii inaitwa zahanati ya Neema tumejenga kwa miaka kumi kwa msaada wa NMB kwa kupata mkopo tumandikishwa kisheria kwasasa tulivyoanza tunatibu kwa mwezi watu 300 lakini tumeweka mikakati kwa kushirikiana na serikali ili tuboreshe zaidi na kuna vyumba hapa tumetoa bure kabisa kwa ajili ya huduma ya mama na mtoto.”Amesema Dokta Nkambi

Akizungumza mmoja wa akina mama aliyefika katika kituo hicho cha afya kupata huduma aliyejitambulisha kwa jina la Mama Mollel amesema kwa muda mrefua wamekuwa wakipata changamoto lakini baada ya kuwepo kwa kituo hicho sasa wanajifungua kwa urahisi zaidi kwa kuwa mwanzo walikuwa wanatembea zaidi ya kilomita 30 kupa huduma ya kujifungua.

Bi Suzan Koila ambaye ni afisa maendeleo ya jamii mstaafu katika halmashauri ya Ngorongoro amempongeza Mbunge Olenasha kwa mikakati aliyoieleza mbele ya wananchi kuhusu ujenzi wa hospitali ya Wilaya pamoja na vituo vya afya ambavyo vitarahisisha zaidi huduma na kufanya afya iboreshwe.

Magufuli amwaga Mabilioni ya Fedha Ngorongoro Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya na vituo vya afya Magufuli amwaga Mabilioni ya Fedha Ngorongoro Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya na vituo vya afya Reviewed by KUSAGANEWS on July 07, 2018 Rating: 5

No comments: