Msafara wa Waziri wa
Maliasili, Dkt. Hamisi Kigwangalla umesimamishwa na kundi kubwa la
wananchi wa kijiji cha Kisumba kilichopo wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa
wakiwa na mabango yanayoeleza kero zao mbalimbali.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akijibu kero
mbalimbali za wananchi wa kijiji cha Kisumba katika wilaya ya Kalambo
mkoani Rukwa baada ya msafara wake kusimamishwa na wananchi hao.
Miongoni
mwa kero hizo ni pamoja na wanyamapori jamii ya Tembo kuvamia mashamba
yao na hivyo kukosa chakula na kukosekana kwa huduma muhimu ya maji
iliyotokana na kuchakachuliwa kwa mradi wa maji wa jumla ya shilingi
milioni 663 kijijini hapo.
Mkazi wa kijiji hicho, Leonard Kiombe amesema mara nyingi wamekuwa wakiwasimamisha viongozi kwa sababu ya kero ya maji, "tulipata
mradi wa milioni 663 wakasema zaidi ya vijiji 6 vitapata maji lakini
kijii cha kisumba mpaka sasa hatuna maji, mradi umechakachuliwa na maji
hayatoki".
Akijibu kero hizo, Waziri Kigwangalla amemuagiza Katibu Mkuu wa
Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha Taasisi za Uhifadhi wa
Wanyamapori pamoja na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS
wanashirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo kutengeneza vikundi
vya wananchi wa vijiji vyote vinavyopakana na Hifadhi ya Msitu wa
Kalambo na Pori la Akiba Lwafi ili wawezeshwe fedha za mikopo ama
mizinga ya kufugia nyuki ambayo wataipanga pembezoni mwa mashamba yao
ili kuzuia tembo wasiingie kwenye mashamba.
"Teknolojia hiyo imethibitika kusaidia kudhibiti tembo
walilete madhara kwenye makazi ya watu kwa kuwa nyuki hufukuza tembo na
endapo tembo nao wakinusa harufu ya nyuki huwa sio rahisi kusogelea
maeneo hayo, hivyo ameagiza mradi huo utekelezwe ndani ya kipindi cha
miezi miwili kabla mvua za masika kuanza", amesisitiza Kigwangalla.
Waziri Kigwangalla pia ametoa wito kwa wananchi hao kuacha kufanya
shughuli zao kwenye maeneo ya hifadhi ikiwemo maeneo ya mapito ya
wanyamapori kwa kuwa kufanya hivyo ni kuhatarisha maisha na ustawi wao
Msafara wa Kigwangalla 'wavamiwa'
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 07, 2018
Rating: 5
No comments:
Post a Comment