Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole
ametumia mkutao wa kampeni za kumnadi mgombea wa chama hicho katika uchaguzi
mdogo Kata ya Turwa kumnanga Mwenyekiti wa (Chadema), Freeman Mbowe
Akihutubia mkutano wa uzinduzi wa kampeni hizo katika
viwanja vya Rebu mjini Tarime jana Julai 29, 2018, Polepole amedai
uking’ang’anizi wa Mbowe katika nafasi ya uenyekiti wa chama hicho ndicho
kinawakimbiza makada na viongozi wake wakiwemo wabunge na madiwani wanaotimkia
CCM
“Kukosa ushirikiano kutoka uongozi wa juu wa chama na
kutoambilika kwa Mbowe ni kati ya sababu zinazowakimbiza wanaohama Chadema.
Natabiria chama kile kuendelea kuporomoka zaidi,” alisema Polepole
“Kuna wabunge wawili ambao kwa sasa nahifadhi majina yao nao
watahamia CCM wakati wowote kuanzia sasa; madiwani wanaoomba kuja idadi yao
haihesabiki,” aliongeza
Akimnadi mgombea wa CCM, Mwita Chacha maarufu Chacha
Kamanda kiongozi huyo aliwaomba wapiga kura wa Kata ya Turwa kumchangua mgombea
huyo ili akashirikiane na viongozi wa CCM inayoongoza Serikali kuwaletea
maendeleo.
Polepole alitumia mkutano huo kutaja baadhi ya miradi
inayotekelezwa ikiwemo ununuzi wa ndege, ujenzi wa reli ya kisasa, elimu bure,
ujenzi wa barabara na madaraja kuwa mfano wa utekelezaji wa ilani na ahadi za
CCM wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2015
Aliyekuwa diwani wa Turwa kupitia Chadema aliyetimkia CCM,
Zakayo Wangwe alitumia mkutano huo kuwaeleza wapiga kura sababu zake za kuhama
ni kukosa ushirikiano kutoka kwa mbunge wa Tarime Mjini, Ester
Matiko akidai alikuwa akipinga kila wazo alilotoa kwa hofu ya yeye kuwania
ubunge 2020
Zakayo ambaye sasa ni Ofisa Mtendaji wa Kijiji katika moja
ya vijiji vya Kata ya Nyamwaga pia alimtuhumu Mbowe hakuwa upande wake kutokana
na historia ya upinzani kati yake na marehemu baba yake, Chacha Wangwe
Mbunge wa Jimbo la Bunda Vijijini (CCM), Born
Getele akimwombea kura mgombea udiwani akisema CCM ndiyo chama imara
kilichomakini kisicho na ubinafsi hivyo kubaki Chadema ni kupoteza muda
Akiomba kura, mgombea Mwita Chacha aliwaomba wapiga kura
kumwamini na kumchagua ili akasimamie utekelezaji wa ilani ya CCM ambayo ndiyo
inatekelezwa licha ya halmashauri na jimbo la Tarime kuongozwa na Chadema
Polepole atangaza kupokea wabunge zaidi wa Chadema
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 30, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 30, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment