Serikali yakabidhiwa cha Mv Mwanza


Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwelwe, amewataka watendaji wa wakala wa ufundi na umeme nchini (TEMESA), kujitathimi katika utendaji wao wa kazi kufuatia kuwepo kwa malalamiko mengi kuhusiana na matengenezo ya magari ya serikali

Mhandisi Isaac Kamwelwe ametoa agizo hilo, wakati akipokea rasmi kivuko kipya na cha kisasa cha MV. Mwanza kilichojengwa  na mkandarasi mzawa kampuni ya Songoro Marine ya Jijini Mwanza, ambacho kimegharimu shilingi bilioni 8.9 za kitanzania, chenye  uwezo wa kubeba abiria 1,000, tani 250 za mizigo na magari 36 kwa wakati mmoja ambacho kitatoa huduma ya usafirishaji kati ya Kigongo - Busisi mkoani Mwanza ndani ya ziwa Victoria

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella pamoja na mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel, wamepongeza juhudi za rais John Magufuli za kuboresha huduma za vivuko katika ziwa Victoria

Naye mwenyekiti wa bodi ya TEMESA Brigedia Jenerali mstaafu Mabula Mashauri amesema wakala huo utahakikisha miundombinu ya usafiri na usafirishaji katika ziwa Victoria unakuwa bora, salama na wenye uhakika
Serikali yakabidhiwa cha Mv Mwanza Serikali yakabidhiwa cha Mv Mwanza Reviewed by KUSAGANEWS on July 30, 2018 Rating: 5

No comments: