Kukosekana kwa Uzio Kambi ya Fungafunga kwasababisha wazee Kutoroka


Kukosekana kwa uzio katika kambi ya wazee wasiojiweza wanaolelewa katika kituo cha Fungafunga kilichopo manispaa ya Morogoro kumetajwa kuwa ni changamo kubwa inayo sababisha wazee hao kutoroka na kwenda kuombaomba barabarani licha ya serikali kuwahudumia wazee hao kwa kila kitu huku vibaka nao wakitumia nafasi hiyo kufanya udokozi wa mara kwa mara katika kambi hiyo

Akizungumza mara baada ya kupokea msaada wa vitu mbalimbali kutoka kwa kikundi cha umoja wa marafiki Kihonda (UMAKI ) mlezi wa wazee hao Tehora Njimba pamoja na kuwashukuru wadau hao lakini pia amesema tatizo la kukosekana kwa uzio ni changamoto kubwa kunako hatarisha ustawi na afya za wazee hao

Kwaupande wao wazee hao wameomba serikali kuwapatia wataalamu kupewa elimu ya ujasiamali ili waweze kuelimishwa kuhusiana na shughuli mbalimbali ikiwemo ufugaji wa Kuku na bustani za Mboga huku mwenyekiti wa kikundi cha UMAKI Peter Tarimo akieleza lengo la kikindi kuwatembelea wazee hao.
Kukosekana kwa Uzio Kambi ya Fungafunga kwasababisha wazee Kutoroka Kukosekana kwa Uzio Kambi ya Fungafunga kwasababisha wazee Kutoroka Reviewed by KUSAGANEWS on July 30, 2018 Rating: 5

No comments: