Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imeweka sheria
kali zinazowalinda watoto wa kike na watakaobainika kuwapa ujauzito na
kukatisha masomo yao adhabu watakayoipata hawatoisahau maisha
Aliyasema hayo jana (Jumapili, Julai 29, 2018) wakati
akizungumza na wakazi wa kata ya Mwakizega wilaya ya Uvinza akiwa katika
ziara yake ya kikazi mkoani Kigoma.
Alisema Serikali itatoa adhabu kali kwa mtu atakayebainika
kukatisha elimu ya mtoto wa kike iwe kwa kumuoa au kumpa ujauzo
Alisema watoto wa kike wanatakiwa kuheshimiwa katika jamii
na waachwa waendelee na masomo yao kwani elimu ni haki yao ya msingi
"Tukikukuta na mwanafuzni wa kike kwenye kona
zisizoeleweka adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka 30 gerezani, hivyo
vijana kuweni makini," alisisitiza
Pia Waziri Mkuu aliwataka wazazi na walezi kushirikiana na
Serikali kuhakikisha watoto wa kike wanapelekwa shule na wanamaliza masomo yao
Waziri Mkuu aliwaasa wanafunzi wote kusoma kwa bidii ili
watimize ndoto zao na wasikubali kushawishika kwa kuwa watashindwa kufikia
masomo yao
Wanaowapa Mimba watoto wa Shule Kukiona Cha Moto
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 30, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 30, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment