Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole
amekanusha taarifa za chama hicho kumpa barua ya onyo mbunge wa Mtama, Nape
Nnauye
Akizungumza leo Alhamisi Julai 5, 2018 Polepole amesema
mbunge huyo wa CCM hajapewa barua ya onyo, kwamba chama hicho tawala kina
taratibu zake
Taarifa za Nape kupewa barua hiyo zimesambaa mitandaoni huku
mwenyewe akikanusha kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter
Taarifa hizo zilitiwa chumvi zaidi baada ya kuhusishwa na
msimamo wa Nape katika suala la Korosho lililoibuka katika Bunge la Bajeti
Nape awaonya wanaomzushia kufukuzwa uanachama
Katika mkutano huo wa Bunge, Nape na wabunge wenzake kutoka
mikoa ya Kusini walipinga uamuzi wa Serikali wa kubadilisha Sheria ya Korosho,
ikiwa ni pamoha na fedha za ushuru wa korosho kwenda katika mfuko mkuu wa
Hazina
Akizungumza baada ya uwasilishwaji wa ripoti ya taasisi ya
Twaweza jijini Dar es Salaam, Polepole amesema chama hicho tawala kina
utaratibu wa vikao linapotokea tatizo la mwanachama wake
"Hapana, chama chetu kina utaratibu wa vikao, sio kutoa
barua tu,” amesema Polepole alipokuwa akijibu swali la MCL Digital
Polepole akanusha CCM kumlima barua Nape
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 05, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 05, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment