Mbunge wa Iringa Mjini Mch. Peter
Msigwa, amedai kwamba mabadiliko ya kumtoa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani,
Dkt Mwigulu Nchemba na kuteuliwa Mh. Kangi Lugola hayawezi kubadili chochote
ndani ya wizara hiyo isipokuwa uchochezi.
Akizungumzia
mabadiliko madogo yaliofanyika katika baadhi wizara mwishoni wa wikiiliyopita,
Mh. Msigwa amesema hakuna chochote atakachokifanya Kangi isipokuwa maneno mengi
yanayoweza kumfurahisha mkuu wake.
"Sitegemei kuona mabadiliko yoyote
kwenye wizara hii zaidi ya uchochezi. Kangi ana maneno mengi ambayo yataweza
kumfurahisha mkuu wake wa kazi lakini si mabadiliko. Lugola huwa ni mti wa
kugeuka geuka hivyo atakuwa mtu wa vichekesho 'so' sioni mabadiliko"
Msigwa.
Akiuzungumzia
utawala wa Mwigulu Nchemba ambaye alichukua wizara hiyo kutoka kwa Charles
Kitwanga, Msigwa amesema hakuna alichokifanya katika Wizara hiyo zaidi ya
kusaidia kuzuia mikutano ya kijamii pamoja na kanuni za nchi.
"Mwigulu hajafanya chochote katika
wizara, kuwepo au kutokuwepo kwenye wizara sitaona tofauti yoyote. Kwenye
Wizara ile Mwigulu alikuwa kama picha kwani katika kipindi chake ndipo ajali za
barabarani zimeongezeka, watu wameokotwa kwenye viroba, Mauaji yameongezeka,
amesaidia sana kuzuia mikutano ya vyama".
Ameongeza
kwamba "Mwigulu
alikuwa anashadadia mambo ya hovyo yanayokwenda tofauti na katiba ya nchi na
kanuni za nchi. Sioni tofauti yake".
Msigwa amponda Kangi, ampa jina
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 05, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 05, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment