Ikiwa ni siku chache tangu Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kutoa maagizo kwa viongozi
kuwajibika na wasisubiri hadi mwenyewe awawajibishe na kutolea mfano wa ajali
zilizofuatana jijini Mbeya.
“Mfano, Mkoa wa Mbeya katika
wiki mbili wamekufa watu 40, majeruhi zaidi ya 100, hakuna hatua
zinazochukuliwa hata ya kuwambia RPC na RTO asijiuzulu.
Au hadi wafe wangapi?
Mpunguzie hata nyota ili ajue damu za watu zinavyouma. Kaanze na RPC Mbeya”,
moja ya kauli ya Magufuli.
Alfajiri
ya leo Julai 5, 2018, Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani Kanda Maalum Dar es
salaam kimezindua Operesheni ya Ukaguzi wa magari, madereva, leseni na vyeti
vya udereva kwa madereva wa mabasi ya Mikoani katika stendi kuu ya Ubungo .
Zoezi
hilo limeongozwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam,
Liberatus Sabas, ambapo amesema kuwa lengo la operesheni hiyo ni kuwafanya
madereva kuacha tabia ya kughushi leseni, kuwahimiza wajiunge na mafunzo
ya udereva katika vyuo vinavyotambulika na serikali.
“Polisi Kanda Maalum Dar es salaam
inawataka Madereva wasio na leseni halali, madereva walevi, pamoja wamilki wa
magari walio na magari mabovu kutoyaruhusu magari hayo kuingia barabarani
hadi yatakapotengenezwa na kukaguliwa”, amesema Kaimu Kamanda.
Kamanda ameongeza kuwa Jeshi la
Polisi halitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa wamiliki, Madereva na
Kampuni za usafirishaji zitakazoenda kinyume na sheria, kanuni na taratibu za
usalama Barabarani.
Kauli ya Magufuli yaliamsha Jeshi la Polisi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 05, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 05, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment