Wananchi wa kijiji cha Ngarasero wakimsikiliza mbunge
wao Wiliam Olenasha katika ziara yake ya kutembelea wananchi
|
Imekuwa ni desturi ya mara kwa mara kwa mbunge huyo
kutembelea wananchi wake kila kata ambapo kila kata amepita mara nne tangu
achaguliwe kuwa muwakilishi wa wananchi Bungeni.
Akizungumza na wananchi wa kata ya Ngaresero pamoja na
kata ya Pinyinyi zilizopo katika wilaya hiyo Olenasha Amesema kuwa yeye ni
mbunge ambaye amechaguliwa na wananchi wanyonge ambao wana changamoto ambazo
pia lazima kama mmbunge azitatue kwa kuwa ndiyo jambo alilotumwa na wananchi
kuwawakilisha.
Amesema kwasasa serikali inayoongozwa na Raisi John
Magufuli imejitofautisha sana na kipindi cha nyuma kwakuwa hata maeneo ambayo
yalisahaulika kwa muda mrefu kwa sasa yameshaanza kupatiwa vipau mbele ikiwemo pia
miradi mikubwa ambayo imepelekwa katika jimbo hilo la Ngorongoro.
Olenasha amesema kuwa tayari kupitia yeye kama mbunge
wananchi wameshaanza kuletewa mradi mkubwa wa barabara ya lami ambao ni wa kihistoria
kutoka Loliondo mpaka mto wa Mmbu kilomita 213 mradi ambao wengi walizani ni
ndoto tayari umeshaanza kujengwa.
“Napenda kuwataarifu wananchi kuwa ujenzi wa barabara ya
lami umeshaanza na shilingi Bilioni 87 zimeshatolewa tayari jambo ambalo wengi
walidhani ni ndoto lakini imewezekana na mradi umeanza kwa ksi kubwa”Alisema
Olenasha
Hata hivyo Olenasha amemshukuru Raisi Dokta Magufuli kwa
kuwapa kipau mbele katika kuletea wananchi wake maendeleo ambapo nje na mradi
huo wa Barabara upo mradi wa Umeme,Afya,maji na Elimu ambapo miradi hiyo
imeshaidhinishiwa fedha kwa ajili ya kuanza mara moja.
Kwa upande wa wananchi ambao wameshiriki mkutano huo wa
Mbunge wamesema kuwa tangu kuanza kwa historia ya Uhuru hawajawahi kupata
mawasiliano hata ya Simu wala kuona kituo cha afya lakini kupitia mbunge wao
wameona mafanikio hayo.
Pamoja na hayo wamesema kuwa mbunge wao amekuwa mstari
wa mbele katika suala la maendeleo kwasababu kila mara anatembea jimboni kwake
licha ya kuwa na changamoto zilizopo lakini wanampa ushirikiano mzuri ili
afanikishe kile ambacho ameshakianza kwa muda mrefu.
"Kinachotakiwa kwa wananchi ni maendeleo tu Siyo Siasa Chafu "Mbunge Olenasha
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 07, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment