Spika wa
Bunge, Job Ndugai amesema amepokea barua kutoka kwa aliyekuwa mbunge wa Ukonga,
Mwita Waitara ya kujivua uanachama wa Chadema na kujiuzulu wadhifa huo
Ndugai amesema
hayo leo Jumatatu, Julai 30 akiwa Ikulu jijini hapa wakati wa hafla ya Rais
John Magufuli kutoa hati za viwanja vilivyopo Dodoma kwa mabalozi 62 wa nchi
mbalimbali na mashirika matano ya kimataifa kwa ajili ya kujenga ofisi na
makazi
“Kwa kuwa
nimeambiwa ninaonekana nchi nzima, napenda nitangaze kuwa leo asubuhi nimepokea
barua kutoka kwa mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara kuwa amejivua
uanachama wa
chama chake na kujiuzulu ubunge’ amesema Ndugai ambaye alikaribishwa kutoa
salamu kutoka Dodoma
Ameongeza
ataiandikia barua Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ili taratibu zifuate
“Kilichobakia
ni kuiandikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa rasmi jimbo la Ukonga liko wazi’
ameseam Ndugai
Waitara alitangaza
kujivua uanachama wa Chadema na kujiunga na CCM Jumamosi iliyopita.
Ndugai atoa neno kujizulu Waitara
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 30, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 30, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment