Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amewataka viongozi,
wanachama, wafuasi na wapenzi wa chama hicho kutotishika na wimbi la viongozi
na wanachama wanaohamia vyama vingine akisema linakipa chama hicho fursa ya
kujiimarisha
“Wale wanaokimbilia vyama vingine wanakiimarisha zaidi chama
chetu kwa sababu kinatupa fursa ya kubaki na viongozi na wanachama wenye
uchungu na nia ya dhati ya kukijenga chama chao,” alisema Mbowe
Akihutubia mkutano wa kampeni kumnadi mgombea udiwani katika
uchaguzi mdogo kata ya Turwa wilayani Tarime jana Julai 29, 2018 Mbowe alisema
Chadema iko imara kulinganisha na wakati mwingine kutokana na kubakiwa na watu
wenye nia ya dhati ya kukipigania
“Wanaofika bei kwa ahadi ya fedha au vyeo waondoke mapema na
ninawahakikishia Chadema itaendelea kuwa taasisi imara zaidi kuliko ilivyo
sasa,” alisema Mbowe
Bila kutaja majina, kiongozi huyo alisema chama hicho
kimewahi kuondokewa na viongozi wa ngazi za juu kiasi cha wengi kudhani
kingeyumba lakini ikawa kinyume chake kwa kuimarika na kupata wabunge, madiwani
na wachama wengi zaidi
Viongozi wa kitaifa waliowahi kujiondoa Chadema ni aliyekuwa
Katibu Mkuu, Dk Wilbrod Slaa na Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa zamani Dk
Amani Walid-Kaborou
Mbowe asema Chadema haitishiki na wanaotimkia CCM
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 30, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 30, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment