Jalada la kesi ya uhujumu uchumi, inayomkabili
Mkurugenzi wa Uthaminishaji Madini ya Almasi na Vito Tanzania, Archard
Kalugendo na mwenzake, bado lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini( DPP) kwa
ajili ya uamuzi
Mbali na Kalugendo, mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo
ni Mthamini Almasi wa Serikali, Edward Rweyemamu ambao ni waajiriwa wa
Wizara ya Madini
Wakili wa Serikali, Halid Nasua amedai leo JUlai 30, 2018
mbele ya Hakimu Mkazi Hamis Ally, wakati kesi hiyo ilipotajwa
Nasua amedai kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa, upeĺelezi
bado haujakamilika na kwamba jalada la shauri hilo lipo kwa DPP kwa ajili ya
kulipitia na kulifanyia uamuzi
Baada ya kueleza hayo aliomba kesi hiyo ipangiwe tarehe
nyingine kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika
ama la
Hata hivyo, wakati upande wa mashtaka wakiomba tarehe
nyingine kwa ajili ya kutajwa, upande wa utetezi ukiongozwa na wakili Ludovick
Nickson na Kabula Swedish uliutaka upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi wao
kwa wakati, kwa sababu wateja wao wanaendelea kusota mahabusu
Hakimu Ally, baada ya kusikiliza hoja hizo aliiahirisha kesi
hiyo hadi Julai 30, 2018 kwa ajili ya kutajwa
Kalugendo na Rweyemamu wanasota mahabusu kutokana na DPP
kuzuia dhamana zao na wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi
wakidaiwa kuisababishia Serikali hasara ya Sh2.4 bilioni
Katika hati ya mashtaka, washtakiwa wanakabilkiwa na shtaka
la kuisababishia Serikali hasara ya Sh2.48 bilioni ambapo wanadaiwa kutenda
kosa hilo kati ya Agosti 25 na 31, 2017 katika maeneo mbalimbali ya mikoa
ya Dar es Salaam na Shinyanga
Washtakiwa hao wanadaiwa kwa pamoja na kwa vitendo
vyao wakiwa wathaminishaji wa almasi wa serikali na waajiriwa wa wizara hiyo
waliisababishia serikali hasara ya Dola za Marekani 1,118,291.43 ambazo
ni sawa na Sh2.48 bilioni
Jalada kesi ya vigogo wa madini lipo kwa DPP
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 30, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 30, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment