NAIBU Waziri wa Viwanda,Biashara na
Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya ameiagiza Bodi ya Mikopo ya Elimu ya
ya Juu nchini kutoa kipaumbele kwa Wahandisi na Mafundi Sanifu.
Akizungumza Jijini Arusha wakati wa kongamano la kwanza la Wahandisi na
Mafundi Sanifu katika kuelekea maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa
bodi ya Wahandisi, Stella alisema mikopo hiyo itawezesha kuongeza idadi kubwa
ya wataalamu hao katika kufanikisha uchumi wa kati wa viwanda.
Alisema mpka sasa takwimu
zinaonyesha mafundi sanifu waosailiwa na bodi hiyo ni 927,Wahandisi 22,226 kati
yao wanawake ni 2,200 ambayo sawa ni asilimia 10.
"Idadi hii ni ndogo sana
ukilinganisha na Rais anavyotamani kuharakisha Tanzaia kuwa na uchumi wa kati
wa viwanda hivyo lazima bodi ya mikopp itoe kipaumbele kwa kada hizi muhimu kwa
maendeleo yanayokusudiwa,"alisema
Mhandisi Stella alisema serikali
inatambua mchango mkubwa wa wataalamu hao katika sekta ya uchumi wa viwanda.
Aidha Stella aliwataka
wataalamu hao kufanya kazi kwa uadilifu na kuzingatia weledi kwani
viwanda vingi vya zamani vilikufa sababu ya baadhi ya wataalam kutokuwa
waadilifu.
Alisema sekta ya viwanda ni muhimili
muhimu katika ukuaji wa uchumi ambapo nchi nyingi zimefanikiwa kupitia viwanda
kama China na Vietinam.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Uhandisi
Prof.Ninatubu Lema alisema viwanda vingi vinategemea mafundi sanifu na
Wahandisi,hivyo hawategemei mwekezaji awekeze kwa kutumia roboti badala ya
nguvu kazi.
Alisema changamoto kubwa iliopo
katoka sekra hiyo ni uchache wa wataalamu hao na kushauri vema serikali
ikawekeza vyuo vikuu,vyuo vya ufundi na shule za Msingi na Sekondari ili
kuzalisha wataalamu wengi zaidi.
Kaimu Msajili wa Bodi ya usajili wa
Wahandisi, Mhandisi Patrick Barozi alisema kongamano hilo ni sehemu ya
maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa bodi hiyo ambapo kilele chake
kinatarajia kuadhimishwa Septemba 5 hadi 7 mwaka huu Mkoani Dodoma.
Alisema kongamano hilo litakuwa
endelevu na linatarajia kufanyika kila mwaka huku makongamano kama gayo
yakifanyika katika mikoa na Kanda mbalimbali nchini.
Aidha alisema uhaba wa wataalamu hao
nchini unaathiri utekelezaji wa haraka wa miradi mikubwa kama ya bomba la
mafuta.
"Kutokana na uhaba huu Bodi
tunatarajia kuleta mafundi Sanifu wa nje ya nchi ili wawafundishe wataalamu wa
hapa nchini, kwani tulio nao ni wachache wanakwamisha utekelezaji wa miradi
mbalimbali,"alisema
NAIBU Waziri wa Viwanda ataka Vipaumbele Vitolewe kwa wahandisi ili Kufikia Tanzania ya Viwanda
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 27, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment