Kupatwa
kwa muda mrefu zaidi kwa kile kilichojulikana kama
"mwezi wa damu" katika karne hii kumewasisimua watu
waliokuwa wakiangalia duniani kote jana Ijumaa (27.07.2018).
Tukio hilo liliingiliana na
kukaribia sana kwa sayari ya Mars na dunia katika muda wa
miaka 15, tukio ambalo ni la kusisimua angani.
Wakati sayari ya mwezi
ambayo huongozana na sayari ya dunia wakati wote,
ikipita taratibu angani, makundi ya watu walikusanyika
duniani kote kuweza kupata kuona tukio
hilo la kipekee ambalo ni nadra.
Mbali na ziwa Magadi,
kilometa 100 kusini magharibi mwa mji mkuu
wa Kenya, Nairobi, jamii ya vijana wa Kimaasai
waliangalia kupatwa huko kwa kutumia teleskopu yenye
nguvu iliyotolewa na familia inayoishi katika
sehemu hiyo.
"Hadi leo nilidhani Mars,
Jupiter na sayari nyingine ilikuwa ni fikira tu za
wanasayansi," Purity Sailepo , mwenye umri wa miaka 16
aliliambia shirika la habari la AFP.
Lakini sasa
nimeiona na naweza kuamini na nataka kuwa
mtaalamu wa mambo ya anga ili kuwaeleza
watu wengine."
Tofauti na kupatwa kwa jua,
watazamaji hawakuhitaji kukinga macho yao kwa
kutumia miwani ili kuweza kutazama tukio hilo
la nadra kutokea. Kwa karibu nusu ya dunia, mwezi
ulikuwa kwa sehemu fulani ama kwa ukamilifu
katika kivuli cha dunia kwa muda wa masaa
sita na dakika 14.
Kipindi cha
kupatwa kamili , kilichofahamika kama "kupatwa kamili",
wakati mwezi uliopoonekana kuwa na giza
zaidi , kilikuwa kwa muda wa saa moja na dakika
43.
Wakati huo huo,
sayari ya mars ilionekana karibu na mwezi
katika anga la usiku, ilionekana wazi kwa
macho.
Watalaamu wa anga ambao wanafanya shughuli
hiyo kwa mapenzi yao tu katika kizio cha
dunia cha kusini walikuwa katika nafasi
nzuri ya kutazama tukio hilo,hususan kusini
mwa Afrika , Australia, na Madagascar, licha ya kuwa
tukio hilo pia lilionekana katika mataifa
ya Ulaya , kusini mwa Asia na Amerika ya
kusini.
Watu wengi watazama tukio hilo
Zaidi ya watu 2,000
ikiwa ni pamoja na watoto wengi wakiwa
na vifaa vya kuona mbali walijikusanya
katika mji mkuu wa Tunisia , Tunis.
"Ninamatumaini
kwamba kupatwa huku kutatuletea furaha na
amani," amesema Karima, mwenye umri wa miaka 46,
bila ya kuondoa macho yake angani.
Hata hivyo , hali
mbaya ya hewa ilizuia kuonekana kwa hali
hiyo katika sehemu kadhaa za dunia.
Mvua
kubwa za majira ya monsuni na mawingu mazito
vilizuwia kuonekana kwa mwezi katika eneo
kubwa la India na majirani zake, maeneo
ambayo yalipaswa kuwa na muonekano mzuri.
Hata
pia , watazamaji waliokuwa na shauku ambao
walijikusanya katika vilima na fukwe za
bahari katika kaunti ya Uingereza ya Dorset
walibaki gizani kutokana na mawingu mazito.Wale
waliojikusanya katika mji mkuu wa Brazil Rio de Janeiro
walikuwa na bahati zaidi, wakiuona mwezi
huo mwekundu katika anga iliyokuwa wazi
wakiwa na simu zao na kamera.
"Nafikiri ilikuwa
nzuri sana, na niliipenda sayari ya Mars
zaidi, ambayo iliweza kuonekana karibu kabisa
na mwezi," amesema Talita Olivera , mwenye umri wa
miaka 34.
sayari ya Mars
ilionekana kuwa kubwa kuliko kawaida na
angavu zaidi, ikiwa kilometa milioni 57.7 kutoka
sayari ya dunia katika mhimili wake kuzunguka dunia.
Kupatwa kamili kwa mwezi kunatokea wakati dunia
ikiwa katikati ya mwezi na jua, na kuzuwia
mwanga wa moja kwa moja kutoka katika
jua ambao kwa kawaida hufanya mwezi kung'ara kwa
rangi nyeupe iliyochanganyika na njano.
Mwezi husafiri kwenda
katika eneo maalum kila mwezi , lakini muelemeo
wa mzunguko wake una maana kwa
kawaida unapita juu au chini ya kivuli
cha dunia, kwa hiyo miezi mingi tunapata mwezi mpevu
bila ya kupatwa.
Wakati sayari hizo
tatu zikiwa katika msitari mmoja , hata hivyo,
hali ya hewa ya dunia inasambaza
mwanga wa buluu kutoka katika jua wakati
ikitoa mwanga mwekundu katika mwezi, na huupa
mwezi rangi ya hudhurungi.
Mwandishi: Sekione Kitojo /
afpe
Mwezi wa damu" wasisimua watazamaji
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 27, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 27, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment