Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema wizara hiyo
haihusiki na kupotea kwa mwandishi wa habari wa Kampuni ya Mwananchi
Communications (MCL), Azory Gwanda
Lugola alitoa kauli hiyo jana, wakati wa mkutano wake na
wanahabari uliofanyika ofisi ndogo ya wizara hiyo jijini Dar es Salaam
Gwanda alitoweka tangu Novemba 21, 2017 nyumbani kwake
Kibiti mkoani Pwani, kilomita 130 Kusini mwa Jiji la Dar es Salaam
Gwanda ni mmoja wa waaandishi wa kwanza kuripoti kwa kina
mfululizo wa mauaji yaliyokuwa yakitekelezwa na watu wasiojulikana katika
vijiji mbalimbali katika wilaya hiyo yaliyowalenga polisi na viongozi wa
vijiji. Wakati wa kutoweka kwa mumewe, mkewe Anna Pinoni alisema watu wanne
wakiwa kwenye gari aina ya Toyota Land Cruiser nyeupe walimchukua Gwanda kutoka
katikati ya mji huo, mahali ambapo hupendelea kukaa na kuondoka naye
Akitoa maelezo baada ya kuulizwa swali na mwandishi
aliyehudhuria mkutano huo aliyehoji juu ya watu kupotea akiwamo Gwanda, Lugola
alisema kutoweka kwa mtu kunaambatana na utata
Swali: Mheshimiwa waziri hivi karibuni kumekuwa na matukio
ambayo sisi waandishi wa habari yanatusumbua mojawapo ni kupotea kwa
mwanahabari mwenzetu, Gwanda ambaye bado hajaonekana tangu atoweke Novemba,
mwaka jana. Nini kinachoendelea, hili unalizungumziaje ili waandishi wa habari
tufanye kazi katika mazingira salama bila kubughudhiwa?
Lugola: Zipo hizo habari. Mtu yupo nyumbani kwake halafu
ametoweka. Sisi (Wizara ya) Mambo ya Ndani hatuingilii uhuru wa mtu au kutoweka
nyumbani kwake. Kila mtu ana uhuru kwa mujibu wa Katiba ya nchi anaweza kutoka
sehemu moja kwenda nyingine bila kuvunja sheria. Waziri Lugola alisema kama
Gwanda alitoweka akiwa nyumbani, wao hawahusiki bali wanahusika kumtafuta mtu
aliyetendewa uhalifu ikiwamo kutekwa akisema katika tukio kama hilo vyombo vya
dola humtafuta mtekaji
“Hawa ambao wanatoweka kwao tu, wanakuwa na sababu nyingi.
Kuna wengine maisha yakiwashinda anaamua kwenda kwingine,” alisema
Lugola azungumzia kutoweka kwa Azory Gwanda, atoa kauli tata
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 07, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 07, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment