Kazi ya mwisho ya Mwigulu akiwa waziri


Leo Jumapili Julai Mosi, 2018 saa 9 alasiri Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi alitangaza mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri yaliyofanywa na Rais John Magufuli, huku Mwigulu Nchemba aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi akiachwa

Kabla ya kutangazwa kwa mabadiliko hayo, Mwigulu alikuwa mkoani Kigoma katika ziara na leo saa 6:14 mchana alitembelea bandari ndogo ya Kibirizi

Akiwa katika bandari hiyo, Mwigulu amesema Serikali ipo tayari kuwarudisha makwao wakimbizi walio tayari

“Hakuna sababu ya kuwaacha wakimbizi kuendelea kukaa nchini wakati wanahitaji kurudi makwao. Wapo wafadhili walio tayari kuwasaidia ili wabaki nchini lakini wafadhili hawa wanapaswa kuielewa tu Serikali. Sasa matatizo yamekwisha katika nchi zao hatuna sababu ya kuwazuia,” amesema

“Kwa wale wanaopenda kutunza wakimbizi waende nchi zenye matatizo ambazo bado watu wanakimbia ila huku kwetu kwa wanaotaka kurudi kwao lugha iwe moja ya kuwarudisha maana ndio sheria ya kimataifa inavyosema.”

Kazi ya mwisho ya Mwigulu akiwa waziri Kazi ya mwisho ya Mwigulu akiwa waziri Reviewed by KUSAGANEWS on July 01, 2018 Rating: 5

No comments: