Kihamia nimepokea taarifa za uteuzi wa Mkurugenzi wa NEC nikiwa ndani ya Basi la Super Video Sikua najua


 Mkurugenzi wa jiji la Arusha Dokta Athumani Kihamia ambaye ameteuliwa hii leo Kuwa mkurugenzi wa tume ya uchaguzi nchini Tanzania NEC amesafiri kwa kutumia basi la kampuni ya Super Video linalofanya safari zake kutoka Dodoma mpaka Arusha majira ya saa kumi ambapo taarifa za uteuzi amezipata akiwa ndani ya basi hilo.

Akizungumza kwa njia ya simu na Kusaga News Kihamia Amesema kuwa akiwa ndani ya basi hilo kuja Arusha alipata meseji pamoja na simu mbalimbali zikimpongeza kwa kuteuliwa huku akiwa hajui kinachoendelea lakini wengi wao walikuwa wanampongeza na kumuambia Hongea Kihamia umeteuliwa kuwa katibu mkuu wa NEC 

Tulipomuuliza kwanini ametumia usafiri wa basi ile hali ana gari ambalo ni maalum kwa ajili ya mkurugenzi amesema kuwa wakati mwingine anachangamana na jamii kuona changamoto wanazokutana nazo pamoja na kuunga mkono juhudi za Dokta Magufuli za kubana matumizi ili pia fedha hizo pia zisaidie wananchi wa hali ya chini

"Leo niliamua kutumia usafiri wa basi kama wananchi wengine na hata sikujua kinachoendelea lakini kutokana na simu nyingi nilizopata ni kwamba nimepokea nikiwa ndani ya basi la Super Video la kutoka Dodoma kuja Arusha"Alisema Kihamia

Pia ameongeza kuwa siyo mara ya kwanza kutumia usafiri wa basi ambapo hata watumishi wake wakati mwingine hutumia usafiri huo huo pale inapowalazimu kushughulikia shughuli za wananchi hivyo kutoa wito kwa viongozi wengine kutojisahau wanapokuwa katika magari yenye hadhi watumie siku moja moja ili waone taabu pia wanazopata wananchi wa hali ya chini.

Kihamia alikuwa Mkoani Dodoma kwa ajili ya kuhudhuria semina za uchaguzi mdogo wa madiwani kwa kata ambazo ziko wazi madiwani wake walijiuzulu hivyo kujiandaa kwa ajiliya marudio.
Hata hivyo Mkurugenzi Kihamia amemshukuru Raisi Dokta Magufuli kwa kumteua na kumuona anafaa katika nafasi hiyo na ameahidi kuitumikia vema
                                         

Kihamia nimepokea taarifa za uteuzi wa Mkurugenzi wa NEC nikiwa ndani ya Basi la Super Video Sikua najua Kihamia nimepokea taarifa za uteuzi wa Mkurugenzi wa NEC nikiwa ndani ya Basi la Super Video Sikua najua Reviewed by KUSAGANEWS on July 01, 2018 Rating: 5

No comments: