Wananchi wamuombea Mbunge wao kwa Mungu kwa kuwaletea mtandao wa Simu /Mawasiliano


 Wananchi wa kata ya Pinyinyi na Ngarasero wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha wamempongeza Mbunge wa Jimbo hilo William Olenasha kwa kuwatatulia changamoto ya Mtandao wa simu ambao kipindi cha nyuma walikuwa hawawezi kuwasiliana kutokana na kukosekana kwa mtandao wa mawasiliano ya Simu.

Wakizungumza wakati wa mahojiano Maalum na Mwandishi wa habari hii wananchi hao wamesema kitu cha kwanza ambacho kwasasa wanajivunia ni kuwepo kwa uborsgaji wa mtandao wa simu ambao umekuja kutokana na Juhudi za Mbunge wao 

“Ni kweli mwandishi ukweli kabisa wakati wa miaka ya nyuma tulikuwa ukitaka kupiga simu unaenda mpaka karatu au Mto wa mbu ambao ni umbali mrefu sana kutoka hapa pinyinyi mpaka huko kwenda kupiga simu lakini sasa hivi Mbunge wetu Olenasha ametuletea mtandao wa halotel sasa tunapiga siunaona hata hapa niliposimama simu yangu Inaita kwahiyo oooi kwakweli sijui huyu mbunge Mungu amsaidie na maisha marefu mana acha tu”Alisema Mwananchi

Akizungumza mmoja wa mwananchi aliyejitambulisha kwa jina la Agnes Mollel amesema kuwa walikuwa hata biashara zao haziendelei kwasababu walikuwa hawana mawasiliano yoyote ya kuwasiliana kata moja mpaka kata nyingine lakini kwasasa wanapiga bila wasiwasi na Mbunge wao amewaahidi kuendelea kuboresha huduma hizo za mawasiliano kuwa bora zaidi.

“Unajua kaka hakuna biashara inayoendelea mahali popote bila kuwasiliana lakini sasa hivi nina uwezo wa kumpigia simu mtu kutoka Arusha anitumie mzigo kwa Gari tu japo mtu hamjuani lakini Simu ndiyo kila kitu mimi sitaki kumpamba mbunge wetu lakini Anafanya kazi nzuri ambayo kweli kila mtu anaiona anapopita tuna mabarabara,maji,huduma za afya zinakuwa nzuri sasa yani Olenasha nika Lulu ambayo tulikuwa tunaitafuta kwa muda mrefu sasa tumeipata nayo sasa tunaona ina ng”aa kweli”Alisema Agnes

Naye mfanyabiashara ya Utalii katika eneo la Ngarasero Heritenson Kiwale amesema kuwa amekuwa akifanya biashara ya watalii lakini tatizo kubwa lilikuwa ni mawasiliano baina yao na watalii lakini kwasasa wanawasiliana hata kama mtu uko ndani ya nyumba unaweza kupiga na kupokea simu hivyo akawaomba wananchi kushirikiana kwa pamoja ili kuboresha zaidi

“Yani niseme labda mimi ni mfanyabiashara wa muda mrefu sana yani labda Tangu uhuru hili eneo hakukuwa na kupiga simu wala kupokea unatoka nayo mjini huko ukija inakaa tu kama kopo lakini sasa hivi nawasiliana na mzungu yuko Canada kwa simu tu yani kweli kumendelea sana”

Kwa upande wa Mbunge William Olenasha amesema kuwa kwa muda mrefu alipokuwa anaomba kura katika kijiji cha Pinyinyi changamoto kubwa ilikuwa ni mtandao wa simu ambapo tayari anaendelea kuboresha zaidi na tayari minara imejengwa na wananchi wanaendelea kupata maendeleo.
“Nimeshaleta minara miwili ambayo mmoja unafanya kazi lakini mwingine unajengwa na umeanza wiki iliyopita katika mlima wa Kilai na halotel wameniahidi ndani ya wiki mbili watakuwa wameuwasha na nitahakikisha kila mahali panakuwa na network”Alisema Olenasha Mbunge
Jimbo la Ngorongoro Lenye kata 28 ambapo umbali wa kutoka kata moja kwenda nyingine ni kiasi cha kilomita zaidi ya 25 lakini kama Mbunge tayari ameshazunguka kata Zote lengo ni kuwasaidia wananchi wake waliompigia kura na kumchagua ili awawaikilishe bungeni.

Wananchi wamuombea Mbunge wao kwa Mungu kwa kuwaletea mtandao wa Simu /Mawasiliano Wananchi wamuombea Mbunge wao kwa Mungu kwa  kuwaletea mtandao wa Simu /Mawasiliano Reviewed by KUSAGANEWS on July 07, 2018 Rating: 5

No comments: