|
Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT
Wazalendo) Zitto Kabwe amesema kitendo cha Waziri wa Mambo ya Nje, Dk
Augustine Mahiga kuonekana akigonganisha glasi na Waziri Mkuu wa Israel,
Benjamin Netanyahu kimemtia aibu
Amesema kitendo hicho huenda
kikaibua tafsiri tofauti kwa Palestina ambao kwa muda mrefu nchi hizo mbili
zimekuwa na mvutano
Akizungumza leo Mei 23, 2018
katika mjadala wa bajeti ya wizara hiyo mwaka 2018/19, Zitto amesema Tanzania
ilijenga heshima ya kupigania haki
kwa wanyonge tofauti na sasa
Tuliweka Mwenge juu ya Mlima
Kilimanjaro ili umulike ndani na hata nje ya nchi na ulete upendo pasipo na
upendo, matumaini pasipo matumaini, heshima palipo jaa dharau. Ndiyo mambo
yaliyopo katika sera ya mambo ya nje,”amesema
Amesema kuanzia mwaka 2016
Tanzania imeona aibu kupigia kura katika majukwaa ya kimataifa ya
kuwaunga mkono wanyonge
Amesema Dk Mahiga alikuwa Israel
wakati akigonganisha glasi na Netanyahu, jambo alilodai kuwa linawaumiza
Wapalestina
“Nchi inaona aibu kulaani mauaji
ya wanyonge walionyanganywa nchi yao. Umeonekana (Mahiga) katika televisheni
ya Israel ukizungumza bila kusema lolote kuhusu wanyonge (Palestina),”
amesema
|
|
Zitto azua jambo bungeni
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 23, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 23, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment