Watoto wawili wenye umri
wa miaka 8-12, wameibuka mashujaa baada ya kuokoa mwili wa mtu mmoja
aliyejulikana kwa jina la Mzee Nampwenge aliyekufa na maji, baada ya kuzama
kwenye bwawa alipokuwa akiogelea huko Namayanga, Naliendelea mkoani Mtwara.
Akizungumza na mwandishi wetu
mwenyekiti wa mtaa wa Namayanga Ally Salum Nayove amesema ni kweli watoto
hao waliotambulika kwa majina ya Faraji Muhibu, na Islam Shaibu, wanaosoma
darasa la nne na mwingine la pili ndio walioweza kujitosa kwenye bwawa hilo ambalo
limejaa maji kutokana na mvua zilizokuwa zikinyesha, na kuutoa mwili huo.
Naye mzee Hamisi
Nahoda ambaye ni rafiki wa karibu wa Mzee Nampwenge aliyekuwa naye
siku ya tukio wakiogelea, amesema kwamba rafiki yake huyo alikuwa anajikumbusha
kuogelea lakini maji yalimzidi na kufariki dunia saa chache kabla ya kufuturu.
Kutokana na tukio hilo mwenyekiti
Ally Salum
Nayove amewataka wananchi
na watoto wadogo kutocheza katika maeneo hayo, ambayo awali yalikuwa ni
machombo ya mchanga na sasa kujaa maji kutokana na mvua.
Watoto watoa mwili wa aliyekufa maji Mtwara
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 23, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 23, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment