Mbunge wa Geita Vijijini Joseph
Msukuma amefunguka na kudai kufarakana kwa chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) na CUF kimesababishwa na mzimu wa Profesa Lipumba na wala sio kitu
kingine ambacho watu wanafikilia.
Musukuma ametoa kauli hiyo wakati
alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara
kupitia ukurasa wa EATV baada ya kuulizwa ni kiongozi gani wa upinzani anayemvutia.
"Mwanasiana wa upinzani
anayenivutia ni Profesa Lipumba anajua hesabu za kuvuruga vyama nampenda sana,
Lipumba yeye na Sakaya ni mabingwa wa kutibua siasa anajua kupiga hesabu za
kuchekecha vyama, hata kufarakana kwa CHADEMA na CUF ni mzimu wa Lipumba
huo", Musukuma.
Pamoja na hayo, Musukuma ameendelea
kwa kusema "Lipumba nampenda kwa sababu ni mvurugaji wa hivi
vyama vidogo vidogo, anaifanyia kazi nzuri sana CCM, yule ni 'master' wa
kuvuruga".
Kwa upande mwingine, Joseph Msukuma
amesema katika maisha yake anatamani awe fundi wa hesabu za siasa za kuvuruga
vyama kama alivyo Prof. Lipumba.
Nampenda Lipumba anajua kuvuruga- Musukuma
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 23, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 23, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment