TAHARUKI YATANDA ROMBO BAADA YA MAREHEMU KUFUFUKA


Taharuki yaibuka kwa Marehemu Aliyefufuka na kumtokea Mkewe
HALI ya Taharuki imewakumba wakazi wa Kijiji cha Leto ,Mamsera wilaya ya Rombo kufuatia tukio la Mkazi mmoja wa eneo hilo aliyekuwa amefariki dunia miezi miwili iliyopita  kuibuka ghafla nyumbani kwake aelezwa kuwa amefufuka. 
  
Marehemu huyo aliyetajwa kwa jina la Richard David Tarimo(28)alifariki kifo cha kutatanisha Marchi 30 mwaka huu baada kula Nyama aliyoletewa na kaka yake aitwaye Senzo David na baadae kuanza kujisikia vibaya na kufariki dunia ghafla wakati akikimbizwa hospitalini kwa matibabu.

Mke wa marehemu alitwaye Mery Richadi anaeleza kuwa siku ya mazishi ya kijana huyo kuliibuka jambo la kushangaza kutokana na udongo uliochimbwa kwenye kaburi hilo kutotoshea wakati wa kufukia ,ndipo padre aliyekuwa akiongoza misa ya kumwombea marehemu  alipohoji kwanini kaburi halijai ,ndipo baadhi ya waombolezaji walipomjibu kuwa haliwezi kujaa kwa sababu marehemu amechukuliwa kimazingara.

Wiki mbili baada ya marehemu kuzikwa amekuwa akimtokea mkewe barabarani mara kwa mara na kumtaka afunge Novena kwani huko aliko anateseka.

Mery anasema kuwa Mey 20 mwaka huu Marehemu mumewe aliibuka ghafla nyumbani kwake, jambo lililomshangaza na watu wengine na kuibua taharuki ya aina yake baada ya kudaiwa kufufuka.

Akisimulia mkasa huo mzito, Mery david alidai kuwa kabla ya kuibuka kwa marehemu mumewe,mara kadhaa amekuwa akimtokea sehemu mbalimbali pindi anapokuwa peke yake na kumweleza kuwa afunge Novena siku tisa kwani huko aliko anaishi kwa mateso makubwa.

‘’Niliamua kufunga Novena na baada ya kumaliza mfungo wa siku tisa ndipo  ghafla akatokea mchungaji mmoja ambaye sikuwa namfahamu na kunieleza kuwa marehemu  mume wako atarejea ‘’Amesema Katika Kaburi la Marehemu Kaburi Alipozikwa Marehemu

Mamia ya wakazi wa kijiji hicho waliokuwa wamefurika nyumbani kwa marehemu alilizingira kaburi la marehemu huyo wakitaka lifukuliwe ili waangalie kilichozika baada ya marehemu kuonekana akiwa hali ndani ya miezi mitatu.

Baba mzazi wa kijana aliyefufuka, Mzee David Kimario ameshangazwa hatua ya kurejea  kwa mwanae uraiani baada ya  kudaiwa kufufuka baada ya kufa, ila amefurahi kumpata tena kijana wake kwa sababu kifo chake kilikuwa cha utata na cha muda mfupi.
 
Ila anachotaka ni kujua mwanaye alikuwa wapi na alikuwa akifanya nini na kwenye kaburi kulizikwa nini.

TAHARUKI YATANDA ROMBO BAADA YA MAREHEMU KUFUFUKA TAHARUKI YATANDA ROMBO BAADA YA MAREHEMU  KUFUFUKA Reviewed by KUSAGANEWS on May 23, 2018 Rating: 5

No comments: