FAMILIA YATAKA MAREHEMU AANDALIWE HARUSI


Familia ya marehemu Confidence Nwanma ya nchini Nigeria ambaye inadaiwa alichomwa kisu na kuuawa na mpenzi wake katika ugomvi wao, familia ya Marehemu sasa imemtaka jamaa huyo kuandaa harusi ya kitamaduni na maiti ya mtoto wao kabla ya mazishi. 

Saliu Ladayo alijisalimisha polisi na kudaiwa kukiri kumuua Confidence katika nyumba yao. Akizungumza na waandishi habari, baba mzazi wa Marehemu, Jude Nwanma amesema kuwa Ladayo lazima achukue mwili wa marehemu na kumpeleka katika kijiji chao ili amuoe kabla kuzikwa. 

Aidha Baba wa marehemu alitoa onyo kali kwa kijana huyo iwapo harusi hiyo haitafanyika.

FAMILIA YATAKA MAREHEMU AANDALIWE HARUSI FAMILIA YATAKA MAREHEMU AANDALIWE HARUSI Reviewed by KUSAGANEWS on May 23, 2018 Rating: 5

No comments: